Botswana yazindua mpango wa mageuzi ya kiuchumi ili kuwa na uchumi wa aina mbalimbali

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2025

Rais Duma Boko wa Botswana akizungumza kwenye hafla ya kuzindua Mpango wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Botswana mjini Gaborone, Botswana, Julai 15, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Rais Duma Boko wa Botswana akizungumza kwenye hafla ya kuzindua Mpango wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Botswana mjini Gaborone, Botswana, Julai 15, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE - Rais Duma Boko wa Botswana amezindua Mpango wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Botswana jana Jumanne, akitoa wito wa mawazo makini kuharakisha ukuaji wa uchumi wa nchi na kusukuma maendeleo ya taifa. Boko amesema kuwa kupitia mpango huo, Botswana inalenga kubadili mazingira yake ya kiuchumi kupitia maendeleo jumuishi na endelevu.

Kwa mujibu wake, mpango huo unalenga kusukuma mpito wa Botswana kwenda katika uchumi wa aina mbalimbali, ulio himilivu na uliounganishwa zaidi kimataifa.

"Mpango huu utaifanya Botswana kuwa nguzo ya kikanda ya shughuli za mambo ya fedha za kuvuka mpaka, kutumia kikamilifu hali yetu ya kuwa na uhakika kisheria, utulivu wa kisiasa, na sifa mzuri," Boko amesema.

Ameeleza kuwa mpango huo unaendana na ilani ya serikali na unahimiza utulivu wa uchumi mkuu na uhimilivu dhidi ya mishtuko ya kimataifa.

"Tutavutia wawekezaji wa ndani na wa kimataifa kwa usahihi, lengo, na mfumokazi wa utekelezaji wa kiwango cha kimataifa," Boko amesema.

Rais huyo ameyasema hayo kwenye hafla hiyo ambayo pia ilitumika kwa ajili ya kuzinduliwa kwa tovuti ya Wito wa Mawazo, sehemu ya kampeni ya wiki nne ya nchi nzima inayoalika mawazo makini, miradi mikubwa, mageuzi ya sekta ya umma, na mapendekezo yenye mchango mkubwa ya kuunga mkono mpango huo.

Uchumi wa Botswana umeendelea kupoteza msukumo katika miaka ya hivi karibuni, ukirekodi ukuaji wa asilimia 3.2 mwaka 2023 lakini ukikabiliwa na makadirio ya kuongezeka kwa asilimia 3.1 mwaka 2024, kutokana na kudhoofika kwa mahitaji ya kimataifa ya almasi na kupungua kwa uzalishaji. Mauzo ya almasi nje ya nchi huchukua asilimia zaidi ya 90 ya jumla ya mauzo yote ya nje ya nchi hiyo, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Benki ya Dunia iliyotolewa mwezi Aprili.

Rais Duma Boko wa Botswana akizungumza kwenye hafla ya kuzindua Mpango wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Botswana mjini Gaborone, Botswana, Julai 15, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Rais Duma Boko wa Botswana akizungumza kwenye hafla ya kuzindua Mpango wa Mageuzi ya Kiuchumi wa Botswana mjini Gaborone, Botswana, Julai 15, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha