China yatoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari

(CRI Online) Julai 16, 2025

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China Lin Jian amesema, China imetoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Nigeria kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari.

Akitoa rambirambi hizo jana Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari, Lin amesema Buhari alikuwa kiongozi muhimu wa Nigeria aliyeongoza watu wa Nigeria kupata mafanikio makubwa katika ujenzi wa nchi.

Aidha, amesema kuwa alikuwa rafiki wa watu wa China na ametoa mchango muhimu katika kukuza uhusiano kati ya China na Nigeria, pamoja na ushirikiano wa kirafiki wa kuungana mkono kati ya nchi hizo mbili.

Mapema siku ya Jumatatu, Rais wa Nigeria Bola Tinubu alitoa taarifa kupitia mshauri wake maalumu akisema, rais wa zamani wa nchi hiyo Muhammadu Buhari amefariki mjini London, Uingereza alikokuwa akitibiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha