Mji wa Shanghai, China wazindua mpango wa visa na motisha za pesa kwa waandaaji maudhui ya mtandaoni duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 16, 2025

Picha hii iliyopigwa tarehe 15 Julai 2025 ikionyesha Bund FTC, mojawapo ya nafasi za umma kwa ajili ya uandaaji maudhui ya mtandaoni yenye ubora wa hali ya juu katika Wilaya ya Huangpu, Shanghai, Mashariki mwa China. (Picha na Cai Weishuai/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa tarehe 15 Julai 2025 ikionyesha Bund FTC, mojawapo ya nafasi za umma kwa ajili ya uandaaji maudhui ya mtandaoni yenye ubora wa hali ya juu katika Wilaya ya Huangpu, Shanghai, Mashariki mwa China. (Picha na Cai Weishuai/Xinhua)

SHANGHAI – Mji wa Shanghai, mashariki mwa China umezindua mpango mpya wa kisera jana Jumanne ili kujiimarisha kuwa kituo cha kimataifa cha uandaaji maudhui ya mtandaoni yenye ubora wa hali ya juu, ikitoa motisha za kifedha, michakato ya visa iliyorahisishwa, na uungaji mkono wa kiteknolojia kuvutia waandaaji maudhui ya mtandaoni kutoka duniani kote.

Mpango huo wa kisera wenye vipengele tisa kinateua maeneo mawili katikati mwa mji huo -- Huangpu na Yangpu -- kama maeneo ya majaribio kwa makundi ya kuandaa maudhui ya mtandaoni duniani, yenye majukwaa, vilea vipaji na maeneo maalum ya kiviwanda yenye ufanisi wa hali ya juu yanayostahiki tuzo ya mwaka ya kiwango cha mji huo ya hadi yuan milioni 10 (dola za Kimarekani takriban milioni 1.4).

Kwa mujibu wa sera hiyo mpya, waandaaji maudhui wa kigeni watafaidika kutoka kwenye michakato ya visa inayoharakishwa, huku maeneo zaidi ya kitamaduni na miundombinu muhimu itafungua milango yao kwa uzalishaji maudhui. Majukwaa ya kimataifa ya waandaaji maudhui na mashindano ya uvumbuzi yataandaliwa ndani ya maeneo hayo ya majaribio.

Mpango huo wa kisera unaeleza kuwa, miradi ya maudhui inayoendeshwa na AI inaweza kupokea uungaji mkono wa mtaji unaogharamia hadi asilimia 30 ya gharama zake, huku waandaaji maudhui wakipokea hadi yuan 100,000 kwa kazi zao bora. Aidha, mpango huo pia unajumuisha mikopo yenye riba ya chini, nafasi za kazi zinazotumika kwa pamoja na makazi kwa watu wenye ujuzi ili kupunguza vizuizi vya kuingia.

Mji huo wa Shanghai umedhamiria kurahisisha uidhinishaji wa kitaalamu kwa waandaaji maudhui, kuhimiza majukwaa ya mtandaoni kushiriki katika tathmini ya ujuzi, na kuboresha njia za ukuzaji taaluma. Aidha, mji huo utaimarisha mifumo ya mafunzo kazini kati ya vyuo vikuu na kazi ya kuandaa maudhui ndani ya vituo vya maudhui na kujumuisha waandaaji maudhui katika miradi ya tuzo za vipaji. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha