

Lugha Nyingine
Rais wa China akutana na wakuu wa ujumbe wa kigeni wanaohudhuria mkutano wa baraza la mawaziri wa mambo ya nje wa SCO
(Picha/Xinhua)
Rais Xi Jinping wa China amekutana na mawaziri wa mambo ya nje na wakuu wa vyombo vya kudumu vya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) jana Jumanne ambao wako Beijing kuhudhuria mkutano wa baraza la mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa SCO.
Rais Xi amesema katika miaka 24 iliyopita tangu kuanzishwa kwake, SCO muda wote imekuwa ikishikilia “Moyo wa Shanghai”, ikikua kuwa shirika lenye nguvu kubwa ya uhai.
Amesema, kuaminiana kisiasa kati ya nchi wanachama kunaendelea kuimarishwa, ushirikiano wa sekta mbalimbali umezaa matunda, huku zikijipatia njia ya ushirikiano wa kikanda inayoendana na mwelekeo wa zama zetu na kukidhi mahitaji ya pande mbalimbali na kuwa mfano wa kuigwa wa uhusiano wa kimataifa wa mtindo mpya.
Amesema, China siku zote inaweka kipaumbele kwa SCO katika diplomasia yake ya ujirani, na imedhamiria kulifanya shirika hilo kuwa imara zaidi, kulinda amani na utulivu wa kikanda, kuhimiza ustawi wa pamoja wa nchi wanachama na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.
Amesema, tangu mwezi Julai mwaka jana, China ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu, imeandaa shughuli mbalimbali, kusukuma mbele ushirikiano, huku pande zote zikichukua hatua thabiti kujenga kwa pamoja maskani bora kwa ajili ya SCO.
Kwenye mkutano ujao wa kilele wa SCO utakaofanyika jijini Tianjin, China, Rais Xi anatarajia kukutana na viongozi wa nchi wanachama, na kujadili kwa pamoja kuhusu mpango wa maendeleo ya Shirika hilo.
Wilaya ya Xuan’en yahimiza utalii wa usiku kando ya Mto Gongshui Katikati mwa China
Eneo la mtaa mkongwe lawa na ustawi kwa uvumbuzi wa kitamaduni na utalii mkoani Jiangxi, China
Mji wa Tianjin, China waharakisha ufungamanishaji wa uchumi wa kidijitali na uchumi halisi
Ardhioevu yalinda spishi za ndege kutoka kwenye uwanda hadi mijini
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma