Waziri wa Mambo ya Nje wa China akutana na mwenzake wa Russia juu ya ushirikiano wa SCO

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 13, 2025. (Xinhua/Yan Yan)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov mjini Beijing, mji mkuu wa China, Julai 13, 2025. (Xinhua/Yan Yan)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amekutana na mwenzake wa Russia Sergey Lavrov jana Jumapili mjini Beijing ambapo Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amemkaribisha Lavrov ambaye yuko ziarani nchini China kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).

"China inapenda kushirikiana na Russia na nchi nyingine wanachama kujiandaa kwa Mkutano wa Kilele wa Tianjin, na kuhimiza maendeleo ya SCO kwenye ngazi mpya," Wang amesema.

Akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, Wang amesema kuwa pande zote mbili zinapaswa pia kufanya shughuli mbalimbali za kumbukumbu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita Vikuu ya Pili vya Dunia (WWII) na kulinda simulizi sahihi ya kihistoria ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Kwa upande wake, Lavrov ameelezea nia ya kushirikiana na China kuzidisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, na kuhimiza uhusiano kati ya Russia na China kupata mafanikio mapya.

"Russia itaendelea kuunga mkono kwa nguvu zote China kuwa nchi mwenyekiti wa zamu wa SCO, kuimarisha mawasiliano na ushirikiano ndani ya mfumokazi wa SCO na mingine, na kuhakikisha mafanikio kamili ya Mkutano wa Kilele wa Tianjin," Lavrov amesema.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu masuala kama vile Peninsula ya Korea, mgogoro wa Ukraine na suala la nyuklia la Iran.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha