Thamani ya biashara kati ya China na Ghana yafikia dola za kimarekani bilioni 11.8 wakati uhusiano wa kibalozi ukitimiza miaka 65

(CRI Online) Julai 10, 2025

Balozi wa China nchini Ghana Tong Defa amesema kwamba biashara kati ya Ghana na China ilikua kwa asilimia 7.1 hadi kufikia dola za kimarekani bilioni 11.8 mwaka 2024.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili siku ya Jumanne, Balozi Tong amesema ukuaji huo mkubwa ni uthibitisho wa uhusiano imara wa kiuchumi kati ya China na Ghana, ambapo China inaendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Ghana na chanzo kikuu cha uwekezaji wa kigeni.

Aidha, balozi huyo amesema kuwa mamia ya kampuni za China zimewekeza katika sekta kama vile miundombinu, viwanda, madini, usafiri wa anga, nishati safi na usafishaji wa mafuta nchini Ghana, zikitoa nafasi nyingi za ajira huku zkiendeleza viwanda vya ndani.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha