Benki Kuu ya Uingereza yaonya juu ya hatari za kiuchumi duniani huku kukiwa na ongezeko la ushuru wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 10, 2025

Askari wa Kikosi cha Household wakitembea kwenye gwaride la Trooping the Color kutoa heshima kwa Mfalme Charles III wa Uingereza wakati wa hafla rasmi ya siku ya kuzaliwa kwake mjini London, Uingereza, Juni 14, 2025. (Picha na Ray Tang/Xinhua)

LONDON - Benki Kuu ya Uingereza (BoE) imeonya jana Jumatano kwamba uchumi wa dunia unakabiliwa na hatari zinazoongezeka, ikitaja kuongezeka kwa ushuru wa Marekani ambapo katika Ripoti yake mpya ya Utulivu wa Mambo ya Fedha, benki hiyo imeonyesha kuwa kuongeza ushuru, hasa wa Marekani, kunapunguza mahitaji ya kimataifa na kuathiri maamuzi ya uwekezaji wa kampuni.

Imeongeza kuwa mivurugiko kwenye minyororo ya usambazaji bidhaa duniani na mivutano ya siasa za kijiografia pia zinazidisha hali ya kutokuwa na uhakika juu ya mfumuko wa bei.

"Masoko ya kifedha yalipitia kipindi cha msukosuko mkubwa mwezi wa Aprili kufuatia Marekani kutangaza sera yake ya biashara," amesema Naibu Meneja wa BoE anayeshughulikia Utulivu wa Mambo ya Fedha Sarah Breeden, akiongeza kuwa hatari na hali ya kutokuwa na uhakika kuhusiana na mivutano ya siasa za kijiografia, vimepunguza ushirikiano katika biashara na sera za kimataifa, na usimamizi wa mambo ya fedha wa serikali duniani kote bado uko juu.

Rais Donald Trump wa Marekani akiongea kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Julai 4, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Rais Donald Trump wa Marekani akiongea kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Julai 4, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

Huku kukiwa na tishio la ushuru, ripoti hiyo imesema madeni ya familia na kampuni duniani bado ni dhaifu.

"Duniani, uwiano wa hesabu za madeni ya familia na ya kampuni unaendelea kuwa mzuri kwa jumla lakini unakabiliwa na changamoto katika muktadha wa mtazamo usio na uhakika wa kiuchumi," imesema.

Picha iliyopigwa Mei 23, 2025 ikionyesha bendera za Umoja wa Ulaya kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Picha iliyopigwa Mei 23, 2025 ikionyesha bendera za Umoja wa Ulaya kwenye makao makuu ya Kamisheni ya Ulaya mjini Brussels, Ubelgiji. (Xinhua/Zhao Dingzhe)

Katika eneo la Euro, ripoti hiyo imetahadharisha kuwa viwanda vya chuma na magari katika eneo hilo "vinazingatia kuuza nje na kwa hivyo ni vyenye kuathiriwa sana na ushuru," na sekta ya magari inapokea sehemu kubwa ya mikopo ya benki.

Kwa mujibu wa Mapitio ya Utulivu wa Mambo ya Fedha ya Benki Kuu ya Ulaya mwezi Mei, misukosuko ya kibiashara inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa uhimilivu wa kampuni za eneo la Euro katika viwanda muhimu vinavyozingatia mauzo ya nje na kwamba kuongezeka kwa misukosuko hiyo ya kibiashara kunaweza kuzorotesha mtazamo wa kampuni, hasa katika sekta ya viwanda.

Kwa upande wa udhaifu wa deni la sekta ya umma duniani, ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa kiwango cha deni katika Pato la Taifa kinaongezeka duniani kote. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha