Trump asema Marekani inabadilisha sera ya Afrika kutoka misaada hadi biashara

(CRI Online) Julai 10, 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na viongozi wa nchi tano za Afrika ambazo ni Gabon, Guinea-Bissau, Liberia, Mauritania na Senegal, katika Ikulu ya White House, akiwaeleza kuwa Marekani inabadilisha sera yake kwa bara hilo kutoka misaada hadi biashara na kusisitiza kuwa Afrika ina uwezo mkubwa wa kiuchumi.

Trump ameongeza kuwa Marekani inajitahidi kutengeneza fursa mpya za kiuchumi zinazohusisha Marekani na nchi nyingi za Afrika. Pia amependekeza kuwa nchi hizo tano zinaweza kuondolewa kwenye mpango wa serikali yake wa kuongeza ushuru wa kutozana sawa kuanzia mwezi Agosti.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, mkutano huo mdogo umepangwa kufanyika kwa siku tatu, huku upanuzi wa upataji wa Marekani wa madini muhimu na maliasili nyingine barani Afrika ukitarajiwa kuwa ajenda ya juu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha