

Lugha Nyingine
China yasema mazoezi ya kijeshi ya Taiwan yatahatarisha tu ustawi wa wakazi wake
BEIJING - Chen Binhua, Msemaji wa Ofisi ya Masuala ya Taiwan ya Baraza la Serikali la China amepinga waziwazi mazoezi mapya ya kijeshi ya Taiwan, akisema kuwa mazoezi hayo yataharibu zaidi amani na utulivu katika Mlango-Bahari wa Taiwan na kuhatarisha usalama na ustawi wa watu wa Taiwan.
Msemaji huyo amesema hayo jana Jumatano wakati akijibu swali la vyombo vya habari kuhusu mazoezi hayo ya kijeshi yaliyoanza jana Jumatano yakihusisha washiriki wengi zaidi na yamepangwa kufanyika kwa muda mrefu zaidi kuliko mazoezi yaliyopita.
Watawala wa Chama cha Kidemokrasia cha Maendeleo (DPP) wameshikilia kwa ukaidi msimamo wao wa mafarakano wa kuifanya "Taiwan ijitenge" na kufuja mara kwa mara rasilimali za umma, wakifanya kwa wapendavyo kuwafunga kihatari watu wa Taiwan kwenye "mkokoteni wa vita vya kuifanya 'Taiwan ijitenge,'" Chen amesema.
Haijalishi watawala wa Taiwan kufanya "mazoezi" kwa mara ngapi, mazoezi hayo hayawezi kubadilisha hali ya kushindwa isiyoepukika kwa "Taiwan ijitenge," wala hayawezi kuzuia mwelekeo wa kihistoria wa muungano wa taifa wa China, msemaji huyo amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma