Maofisa wa Umoja wa Afrika wasema mpango wa Soko la Umeme la Afrika umepata msukumo

(CRI Online) Julai 01, 2025

Maofisa wa Umoja wa Afrika wamesema, mpango wa Soko Moja la Umeme la Afrika (AfSEM), wenye lengo la kuunganisha nchi wanachama wote 55 wa Umoja wa Afrika (AU) kupitia soko la umeme lenye tija na bei nafuu, unaendelea vizuri.

Mwenendo huo wa soko umeelezwa mjini Addis Ababa kwenye mkutano wa kiufundi wa ngazi ya juu uliofanyika jana Jumatatu kuhusu mpango huo, na mpango kabambe wa mfumo wa Umeme wa Bara la Afrika.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Miundombinu na Nishati katika Kamisheni ya ya Umoja wa Afrika (AU) Bw. Kamugisha Kazaura, amesema msingi wa kitaasisi na kiuendeshaji umewekwa kwa ajili ya soko hilo la umeme la Afrika, ambalo linatoa nishati safi, ya uhakika na ya bei nafuu katika bara zima.

Amekumbusha kuwa zaidi ya watu milioni 600 barani Afrika bado hawana huduma ya umeme, na kutoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na endelevu ili kukidhi mahitaji ya nishati yanayokua kwa kasi barani Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha