Shirika la Ndege la Kenya lataka mashirika ya ndege ya Afrika kushirikiana ili kuongeza mapato

(CRI Online) Julai 01, 2025

Shirika la Ndege la Kenya limesema mashirika ya ndege barani Afrika yanapaswa kushirikiana ili kuongeza mapato na kufungua mustakabali wa sekta ya usafiri wa anga katika bara la Afrika.

Mkuu wa Shirika hilo Bw. Allan Kilavuka, amewaambia wanahabari mjini Nairobi jana Jumatatu kwamba ushirikiano kati ya mashirika ya ndege unaweza kusaidia kupunguza gharama za jumla za usafiri wa ndege.

Amesema mashirika ya ndege ya Afrika ni madogo sana ikilinganishwa na mengine ya kimataifa, hivyo yanapaswa kushirikiana badala ya kushindana ili kuhakikisha yanapata faida.

Amesema Shirika la Ndege la Kenya limeanzisha Kundi la Mashirika ya Ndege la Afrika na kuanzisha majadiliano yasiyo rasmi na watoa huduma wengine wa usafiri wa ndege barani Afrika, wanaotaka kujumuishwa ili kunufaika kiuchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha