Baraza la Usalama la UN larefusha muda wa vikwazo dhidi ya DRC

(CRI Online) Julai 01, 2025

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) jana Jumatatu limepitisha azimio la kurefusha muda wa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa mwaka mmoja zaidi hadi tarehe 1 Julai 2026.

Azimilo hilo la Baraza la Usalama lililorefushwa linaweka vikwazo vya silaha kwa makundi yenye silaha nchini DRC, marufuku ya kusafiri kwa watu binafsi na kuzuia mali kwa watu binafsi na mashirika yaliyotajwa na kamati ya vikwazo ya DRC.

Azimio hilo namba 2783 lililoungwa mkono kwa pamoja na nchi 15 wajumbe wa Baraza la Usalama, pia limeamua kurefusha muda wa jopo la wataalam wanaosaidia Kamati ya Vikwazo ya DRC hadi tarehe 1 Agosti 2026.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha