

Lugha Nyingine
Rais Trump atia saini amri ya kuondoa sehemu kubwa ya vikwazo dhidi ya Syria
Msemaji wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Juni 30, 2025. U.S. (Xinhua/Hu Yousong)
WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump ametia saini amri ya mambo ya utawala jana Jumatatu ya kuondoa sehemu kubwa ya vikwazo dhidi ya Syria, Ikulu ya White House ya Marekani imesema katika waraka wa maelezo ya hali, ambapo kufuatia amri hiyo, amri tano za mambo ya utawala kuhusu vikwazo dhidi ya Syria zimefutwa mara moja, huku Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ikitoa msamaha wa siku 180 kwa vikwazo chini ya Sheria ya Kaisari.
"Amri inaondoa vikwazo dhidi ya Syria huku ikidumisha vikwazo kwa Bashar al-Assad (rais wa zamani wa Syria aliyeondolewa madarakani). Amri inaruhusu kulegeza udhibiti wa mauzo ya nje kwa bidhaa fulani na kuondoa vizuizi kwa msaada fulani wa nje ya nchi kwa Syria," imesema Ikulu ya White House.
Wizara ya Fedha ya Marekani tayari imechukua hatua ya kwanza ya kuondoa vikwazo dhidi ya Syria kwa kutoa leseni ya jumla, inayojulikana kama GL25, ili kuidhinisha miamala inayohusisha serikali ya mpito ya Syria, benki yake kuu na viwanda vya kiserikali.
"Vikwazo dhidi ya Assad, washirika wake, wakiukaji haki za binadamu, walanguzi wa dawa za kulevya, watu wanaohusika na shughuli za silaha za kemikali, ISIS na washirika wao na washirika wa Iran vitaendela kuwepo," Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt amesema.
Chini ya amri hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio anaelekezwa "utafuta njia za kuondoa vikwazo katika Umoja wa Mataifa." amesema.
Rubio pia ameelekezwa kupitia tena maamuzi ya kuiweka Syria kuwa "nchi ya ugaidi ya tarehe nane Disemba 2024" , kuweka Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) kuwa shirika la kigeni la kigaidi, na kiongozi wake, mkuu wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa kuwa "Gaidi Aliyebainishwa Maalumu Duniani."
Utawala wa Trump "utaendelea kufuatilia maendeleo katika vipaumbele muhimu" ikiwemo hatua za kurejesha hali ya kawaida ya uhusiano na Israeli na kusaidia Marekani kuzuia kuzuka tena kwa ISIS, taarifa ya White House inasomeka.
Katika wakati wa msukosuko wa Mashariki ya Kati, Rais Trump alimwambia al-Sharaa nchini Saudi Arabia mwezi Mei kwamba Marekani itaondoa vikwazo na kuangalia namna ya kurejesha hali ya kawaida ya uhusiano na kuifanya kuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya kisera.
Kituo cha mafunzo cha Bajiquan mkoani Hebei, China chakaribisha wanafunzi kutoka Russia
Picha: Mandhari ya mbuga katika majira ya joto mkoani Gansu, China
Bustani ya Kimataifa ya Pump Track ya Shenyang, China: Utambulisho Mpya wa Michezo Mjini
Ukumbi wa Kuutazama Mji wa “Kilele cha Tianjin” wa China wafunguliwa rasmi kwa umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma