Sekta ya viwanda ya China yashuhudia nguvu kubwa zaidi wakati inapobadilisha muundo wake kwa madhubuti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2025

Mikono ya roboti ikifanya kazi kwenye karakana ya kampuni ya kutengeneza vipuri vya magari katika Wilaya ya Feixi ya mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Machi 31, 2025. (Picha na Xu Yong/Xinhua)

Mikono ya roboti ikifanya kazi kwenye karakana ya kampuni ya kutengeneza vipuri vya magari katika Wilaya ya Feixi ya mji wa Hefei, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Machi 31, 2025. (Picha na Xu Yong/Xinhua)

BEIJING - Sekta ya viwanda ya China ilipata nguvu kubwa zaidi mwezi huu, huku viwanda vingi zaidi vikirudi katika hali ya ukuaji na uzalishaji wa teknolojia ya hali ya juu na bidhaa za wanunuzi ukiendelea kuwa imara, takwimu za Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zimeonyesha jana Jumatatu.

NBS imesema katika taarifa yake kwamba, kiwango cha wasimamizi wa ununuzi (PMI) kwa sekta ya viwanda nchini China kilipanda kwa mwezi wa pili mfululizo mwezi Juni kufikia 49.7, kikiwa kilikuwa 49.5 mwezi Mei na 49 mwezi wa Aprili.

Imesema kuwa, kati ya viwanda 21 vilivyofuatiliwa, 11 vilirekodi upanuzi mwezi huu, kutoka 7 mwezi Mei na kwamba PMIs kwa utengenezaji wa vifaa, bidhaa za hali ya juu na bidhaa za wanunuzi zimeendelea kuwa katika eneo la upanuzi kwa miezi miwili mfululizo, zikisimama 51.4, 50.9, na 50.4, mtawaliwa.

"Usomaji wa PMI juu ya 50 unaonyesha kuongezeka, wakati usomaji chini ya 50 unaashiria kupungua." imeeleza.

Takwimu hizo za Jumatatu pia zimeonyesha kuwa PMI isiyotokana na viwanda ilikuwa 50.5 mwezi Juni, ongezeko la asilimia 0.2 kuliko mwezi uliopita, na PMI ya jumla ilipanda kutoka 50.4 hadi 50.7.

Hasa, sekta ya ujenzi ilipata nguvu kubwa zaidi ya kufufuka, wakati huohuo sekta ya huduma iliendelea na mwelekeo wake wa kupanda, huku huduma za posta, teknolojia ya upashanaji habari na huduma za kifedha zikidumisha viwango vya juu vya shughuli.

“Huku viwango vyote vitatu vikuu vikiongezeka, hali ya jumla ya uchumi iliendelea kuboreka,” mwanatakwimu wa NBS Zhao Qinghe amesema.

Uchumi wa China ulikua kwa asilimia 5.4 katika robo ya kwanza ya 2025 kuliko mwaka uliopita wakati kama huo, ambayo ni juu kuliko asilimia 5 ya kiwango cha ukuaji wa mwaka mzima kilichorekodiwa mwaka 2024. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha