Xi asisitiza kuimarisha mienendo kwa kuhimiza Chama kijiendeshe kwa nidhamu kali katika mambo yote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2025

BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) jana Jumatatu alipoongoza semina elekezi ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC kilichofanyika siku moja kabla ya maadhimisho ya kuanzishwa kwa CPC alisisitiza kujitahidi kuwa na mienendo mizuri ili kuhimiza Chama kijiendeshe kwa nidhamu kali katika mambo yote.

Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, Xi ametoa salamu za Siku ya Tarehe Mosi Julai kwa wanachama wote wa Chama kote nchini, na baada ya kusikiliza ripoti ya kazi na kushiriki katika mijadala, alitoa hotuba kuhusu kufuata na kutekeleza vitendoni kanuni nane za kamati kuu ya Chama juu ya kurekebisha mienendo.

Xi ambaye pia ni Rais wa China, amedhihirisha kuwa kanuni hizo nane ni hatua za Chama za kujipatia imani ya raia, ni hatua za alama za kujiendesha na kusimamia Chama katika zama mpya.

Amesema tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya CPC mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC imekuwa ikishikilia kanuni kali na kujizuia kwa nidhamu kali katika kurekebisha hali ya utendaji wa kazi na kufanya marekebisho mbalimbali, kupambana na urasimu, utawala msonge, anasa na ufujaji kwa kupitia kampeni za elimu na mfululizo wa hatua za kurekebisha.

"Jitihada hizi zimeboresha kwa ufanisi usimamizi wa Chama na kukusanya nishati chanya kubwa kwa maendeleo ya Chama na mambo ya nchi,” Xi amesema.

Xi amesisitiza kwamba jukumu linalobebwa na Chama la ujenzi wa mambo ya kisasa ya China ni kazi kubwa na ngumu, na utawala wa nchi unakabiliwa na mazingira yenye utatanishi zaidi, hivyo ni muhimu zaidi kwa Chama kujifanyia mapinduzi.

"Viongozi wakuu, hasa makada waandamizi, lazima watangulie kujifanyia mapinduzi," Xi ameongeza.

Amesisitiza kwamba kujifanyia mapinduzi kunahitaji kufuata zaidi nia ya Chama, kushikilia matumaini na imani, kufuata maadili na mwenendo mema.

Kuhusu kupambana na ufisadi, Xi amesema lazima kudhibiti uendeshaji wa madaraka kwa mchakato mzima wa usimamizi, na kuchunguza kwa makini ukiukaji wa nidhamu na sheria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha