

Lugha Nyingine
Wang Yi akutana na Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India
Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa ofisi wa Kamisheni ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na Shri Ajit Doval, mshauri wa usalama wa taifa wa India na mwakilishi maalum wa suala la mpaka kati ya India na China, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Juni 23, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
BEIJING - Mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi amekutana na Ajit Doval, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa India na Mwakilishi Maalum wa India kuhusu suala la mpaka kati ya China na India, mjini Beijing jana Jumatatu akisema kwamba maafikiano muhimu ya kuboresha uhusiano wa pande mbili yalifikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili wakati wa mkutano mjini Kazan, Russia mwaka jana.
Wang, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamisheni ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya CPC, amesema China na India zinapaswa kutilia maanani maafikiano muhimu kwamba ni fursa kwa maendeleo ya kila mmoja na si tishio kwa kila mmoja, na kwamba ni washirika, badala ya mahasimu.
Wang amesema China na India zinapaswa kushikilia mwelekeo wa ujirani mwema na urafiki, kujitahidi kutimiza kunufaishana, kuonyesha hekima ya kihistoria ya staarabu hizo mbili za kale, kushughulikia ipasavyo masuala nyeti, na kudumisha amani na utulivu katika maeneo ya mpakani.
Kwa upande wake Doval amesema kuwa maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi hao wawili yaliweka dira ya uhusiano wa pande mbili, akiongeza kuwa malengo ya kimkakati ya India na China yanaendana, huku maendeleo yakiwa ni kipaumbele cha juu cha nchi hizo mbili.
“India inapenda kuimarisha uratibu na China katika nyanja za pande nyingi, inaiunga mkono kikamilifu China, ambayo ni mwenyekiti wa zamu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), katika kuandaa kwa mafanikio mkutano wake wa kilele, na inaamini kuwa nchi hizo mbili kubwa za Asia zinaweza kutoa mchango mkubwa zaidi kwenye jumuiya ya kimataifa,” Doval ameongeza.
Kuendeleza urithi wa utamaduni usioshikika wa China - ustadi wa kutengeneza chai ya Taiping Houkui
Njia mpya za uendeshaji wa droni zaanza kutumika katika Mji wa Wuhan katikati mwa China
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma