

Lugha Nyingine
Mkuu wa UN aeleza wasiwasi wake juu ya mashambulizi ya droni mjini Port Sudan
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake mkubwa juu ya mashambulizi ya hivi karibuni ya droni mjini Port Sudan, kituo kikuu cha kuingiza misaada ya kibinadamu nchini Sudan, akisema kwamba yanatishia kuongeza mahitaji ya kibinadamu na kutatiza shughuli za misaada nchini humo.
Akiongea kwenye mkutano na waandishi wa habari wa mara kwa mara katika wiki, naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq, amesema katibu mkuu ameonya kwamba ongezeko hilo kubwa la mashambulizi linaweza kusababisha vifo vingi vya raia na uharibifu zaidi wa miundombinu muhimu.
Pia ameeleza kuwa, Guterres anasikitishwa na kupanuka kwa mgogoro huo hadi eneo ambalo limekuwa kimbilio la watu wengi waliokimbia mji mkuu, Khartoum na maeneo mengine.
Tangu Januari, mashambulizi yanayoongezeka nchini kote kwenye vituo vya umeme na miundombinu mingine muhimu yamefanya raia washindwe kupata huduma za umeme, afya, maji safi na chakula.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma