

Lugha Nyingine
Rais Xi atoa wito kwa China na Russia kudumisha azma na uratibu wa kimkakati
![]() |
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin wakifanya mazungumzo ya chai katika ofisi ya rais ya Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia, Mei 8, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi) |
MOSCOW - Rais Xi Jinping wa China jana Alhamisi wakati wa mazungumzo ya chai na Rais Vladimir Putin wa Russia katika ofisi ya rais ya Ikulu ya Kremlin mjini Moscow amesema kwamba China na Russia zinapaswa kudumisha azma na uratibu wa kimkakati wakati dunia ikiingia katika kipindi kipya cha msukosuko na mageuzi.
“Ilimradi tu China na Russia zitadumisha azma na uratibu wa kimkakati, hakuna nguvu inayoweza kuzuia nchi hizo mbili kupata maendeleo na ustawi, hakuna nguvu inayoweza kutikisa msingi imara wa urafiki wa muda mrefu kati ya watu wa nchi hizo mbili, na hakuna nguvu inayoweza kurudisha nyuma mwelekeo uliopo kuelekea dunia yenye ncha nyingi na utandawazi wa kiuchumi,” amesema Rais Xi.
Rais Xi pia ameeleza nia yake ya kuendelea na mawasiliano ya karibu na Rais Putin ili kuweka dira kwa uhusiano kati ya China na Russia na kutoa mchango kwa ajili ya kusongesha mbele usimamizi wa dunia.
Kwa upande wake, Rais Putin amesema kuwa Russia na China siku zote zimekuwa zikisimama pamoja katika mshikamano na kuungana mkono, zikijenga urafiki usioweza kuvunjika.
Rais Putin amesema angependa kudumisha mawasiliano ya karibu ya kimkakati na Rais Xi, kutoa mwongozo wa kimkakati kwa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili, kwa pamoja kukabiliana na changamoto za mazingira magumu ya kimataifa, kuzidisha uratibu wa kimkakati wa pande zote, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili na kuhimiza maendeleo ya dunia yenye ncha nyingi iliyo na usawa na ya kidemokrasia zaidi.
Wakuu hao wa nchi pia wamebadilishana maoni kuhusu mgogoro wa Ukraine na masuala mengine, ambapo Rais Xi amesema kuwa China inatetea na inashikilia maono ya usalama wa pamoja, jumuishi, wa ushirikiano na endelevu katika ngazi ya dunia, na anaamini ni muhimu kutilia maanani kwa uzito masuala halali ya kiusalama yanayofuatiliwa na nchi zote na kuondoa sababu kuu za mgogoro wa Ukraine.
"China inakaribisha juhudi zote zinazosaidia kupata amani na inatazamia kufikia makubaliano ya amani ya haki, ya kudumu na yenye kufuna kisheria juu ya mgogoro wa Ukraine ambayo yanakubaliwa na pande zote husika kupitia mazungumzo," Rais Xi amesema.
Putin amepongeza sana msimamo wa China usio wa upendeleo juu ya utatuzi wa kisiasa wa mgogoro huo wa Ukraine, akisema kuwa Russia inapenda kuanzisha mazungumzo ya amani bila masharti na inatumai kufikia makubaliano ya amani ya haki na ya kudumu.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma