

Lugha Nyingine
Rais Xi asema China na Russia zinapaswa kubeba wajibu maalum za nchi kubwa
Rais wa China Xi Jinping akipeana mkono na Rais wa Russia Vladimir Putin katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia, Mei 8, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
MOSCOW - Katika kukabiliana na hali ya mwelekeo kinzani wa uamuzi wa upande mmoja na vitendo vya umwamba duniani, China itashirikiana na Russia kubeba wajibu maalum zikiwa nchi kubwa za dunia na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Rais wa China Xi Jinping amesema jana Alhamisi wakati akifanya mazungumzo na Rais wa Russia Vladimir Putin katika ziara yake ya kiserikali nchini humo.
Viongozi hao wawili wamebadilishana maoni kwa kina kuhusu uhusiano kati ya China na Russia na masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, wamekubaliana kwa kauli moja kuimarisha ushirikiano wa kimkakati bila kuyumbayumba na kuhimiza maendeleo mazuri ya utulivu ya kiwango cha juu ya uhusiano kati ya China na Russia.
Viongozi hao wawili pia wametoa wito wa kuhimiza mtazamo sahihi wa kihistoria kuhusu Vita vya Pili vya Dunia, kudumisha mamlaka na heshima na hadhi ya Umoja wa Mataifa, na kulinda haki na usawa wa kimataifa.
Kufuatia hafla kubwa ya kumkaribisha Rais Xi, viongozi hao wawili walifanya mazungumzo ya vikundi vidogo na vikubwa mtawalia.
Rais Xi amesema, katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Russia umefurahia maendeleo mazuri ya utulivu ya kiwango cha juu kutokana na juhudi za pamoja za pande zote mbili. Urafiki na ujirani mwema wa muda mrefu na ushirikiano wa kunufaishana umekuwa sifa maalum za uhusiano huo wa pande mbili.
Rais Xi amesema historia na hali halisi ya hivi sasa vimethibitisha vya kutosha kwamba kuendelea kustawisha na kuzidisha uhusiano kati ya China na Russia ni kurithisha haki inayostahiki ya urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili kutoka kizazi hadi kizazi, na ni chaguo lisiloepukika kwa pande zote mbili kufikia kufanikishana na kuhimiza maendeleo na ustawi wao wenyewe.
"Pia ni wito wa zama tulizonazo kwa ajili ya kulinda haki na usawa wa kimataifa na kuhimiza mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa dunia," Rais Xi amesema.
Akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kupatikana ushindi wa Vita vya Watu wa China vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, Vita Vikuu vya Kulinda Nchi vya Umoja wa Kisovyeti na Vita vya Dunia vya Kupinga Ufashisti, katika miaka 80 iliyopita, watu wa China na Russia walijitoa mhanga mkubwa na kupata ushindi mkubwa, wakitoa mchango mkubwa ulio wa alama ya kihistoria kwa ajili ya kulinda amani ya dunia na mambo ya maendeleo ya binadamu.
Rais Xi amesema, haijalishi namna gani mazingira ya nje yanavyobadilika, China itashughulikia kithabiti mambo yake yenyewe, na aliongeza kuwa China inapenda kushirikiana na Russia katika kubeba wajibu maalum unaoletwa na zama.
Kwa upande wake, Putin amekaribisha kwa moyo mkunjufu ziara hiyo ya Rais Xi nchini Russia na kushiriki kwake katika sherehe za kuadhimisha miaka 80 tangu kupatikana ushindi katika Vita Vikuu vya Kulinda Nchi vya Umoja wa Kisovyeti.
Amesema uhusiano kati ya Russia na China unawekwa kwenye msingi wa usawa na kuheshimiana, haulengi upande wowote wa tatu wala hauathiriwi na tukio lolote au wakati wowote. Rais Putin amesema, kutoza kodi ya juu hakuna mantiki na ni kinyume cha sheria, na kutarudisha athari kwa aliyeuweka. Aliongeza kuwa pande mbili Russia na China zinapaswa kuimarisha uratibu na ushirikiano ndani ya mifumo ya pande nyingi.
Akibainisha kuwa Russia na China zilijitolea mhanga mkubwa katika Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, Putin alisema, chini ya uongozi madhubuti wa Chama cha Kikomunisti cha China, watu wa China walipigana kishujaa na kupata ushindi mkubwa katika Vita vya Kupambana na Uvamizi wa Japan, na kutoa mchango mkubwa katika ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia.
Putin amesema, wakati wa miaka hiyo migumu ya vita, Russia na China ziliungana mkono na kujenga urafiki wa dhati, zikiweka msingi thabiti wa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili. Aliongeza kuwa pande zote mbili zinapaswa kulinda mamlaka na heshima ya Umoja wa Mataifa na sheria ya kimataifa, kuhifadhi simulizi sahihi ya kihistoria kuhusu Vita vya Pili vya Dunia, kushikilia haki na usawa wa kimataifa, na kufanya juhudi za pamoja za kujenga mustakabali mwema kwa nchi zote mbili na dunia.
Rais wa Russia Vladimir Putin akifanya hafla ya kumkaribisha Rais wa China Xi Jinping kwenye Ukumbi wa St. George katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia, Mei 8, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
Rais wa China Xi Jinping akiingia kwenye Ukumbi wa St. George katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia, Mei 8, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin wakiingia kwenye ukumbi wa mazungumzo yao katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia, Mei 8, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin wakifanya mazungumzo ya kikundi kidogo katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia, Mei 8, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Russia Vladimir Putin wakipeana mikono baada ya kutia saini taarifa ya pamoja juu ya kuendeleza kwa kina uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Russia wa zama mpya baada ya mazungumzo yao katika Ikulu ya Kremlin mjini Moscow, Russia. (Xinhua/Wang Ye)
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma