

Lugha Nyingine
Rais Xi asisitiza kukusanya nguvu ya umma na tabaka la wafanyakazi kwa kuhimiza ustawishaji wa Taifa la China
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye Mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kuwasifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Li Xueren)
Beijing - Rais wa China Xi Jinping jana Jumatatu kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa, ametoa wito wa kukusanya nguvu ya tabaka la wafanyakazi na watu wengi wanaofanya kazi wa China, na kubadilisha mpango mkuu wa kufikia ustawishaji wa Taifa la China kuwa hali halisi kwa kupitia juhudi zao za kufanya kazi ngumu.
Kwa niaba ya Kamati Kuu ya CPC, Rais Xi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amewapongeza watunukiwa na kutoa salamu zake kwa wafanyakazi, wakulima, wasomi na watu wengine wanaofanya kazi wa makabila yote, vilevile mashirikisho ya wafanyakazi ya ngazi zote na watu wote wanaoshughulikia kazi za mashirikisho ya wafanyakazi kabla ya kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi.
Rais Xi amebainisha kuwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China limeandika ukurasa mzuri katika harakati za wafanyakazi katika miaka 100 iliyopita tangu kuanzishwa kwake.
"Tangu Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC mwaka 2012, mashirikisho ya wafanyakazi ya ngazi zote yamekuwa na mshikamano na wafanyakazi wote na kuwahamasisha kutoa mchango mkubwa katika kufanikisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora kwa pande zote na kuendeleza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China," Rais Xi ameongeza.
Amesema, haijalishi namna gani hali ya kihistoria na makundi ya kijamii yanavyobadilika, hadhi na nafasi ya tabaka la wafanyakazi nchini China, kanuni ya msingi ya kutegemea tabaka la wafanyakazi kwa moyo wote, na asili na kazi za mashirikisho ya kitaifa ya wafanyakazi ya China havitaweza kutetereshwa.
Amesisitiza kuwa katika miaka 100 iliyopita, mafanikio makubwa zaidi katika uvumbuzi wa kinadharia na maendeleo ya kivitendo ya lengo kuu la harakati za wafanyakazi wa China yamekuwa yakiundwa kuwa njia ya maendeleo ya mashirikisho ya wafanyakazi ya ujamaa wenye umaalum wa China
"Kwenye safari mpya katika zama mpya, ni muhimu kuweka mkazo zaidi katika kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya juu na kuhamasisha watu wote wanaofanya kazi kuendelea na juhudi kubwa zaidi ili kupata mafanikio na kuwa wavumbuzi na wabunifu," amesema.
Rais Xi ametoa wito kwa jamii nzima kujifunza kutoka kwa wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa, na kutukuza sifa zao bora, na wafanyakazi hao wa kupigiwa mfano na watu hao wa mfano wa kuigwa wanapaswa pia kuthamini heshima ambayo wamepokea, na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia mafanikio mapya.
Mkutano huo uliongozwa na Waziri Mkuu wa China Li Qiang. Viongozi waandamizi Zhao Leji, Wang Huning, Ding Xuexiang na Li Xi walishiriki kwenye shughuli husika, na Cai Qi alisoma pongezi kwa watu wa mfano wa kuigwa.
Jumla ya watu 1,670 walisifiwa kuwa wafanyakazi wa mfano wa kuigwa wa kitaifa, na wengine 756 wametambuliwa kuwa watu wa mfano wa kuigwa.
Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akitoa hotuba muhimu kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, katika mji mkuu wa China, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Yan Yan)
Xi Jinping, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Cai Qi, Ding Xuexiang na Li Xi wakihudhuria kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali wakitoa vyeti vya heshima kwa wajumbe wa watunukiwa kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali wakitoa vyeti vya heshima kwa wajumbe wa watunukiwa kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Li Xueren)
Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali wakitoa vyeti vya heshima kwa wajumbe wa watunukiwa kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali wakitoa vyeti vya heshima kwa wajumbe wa watunukiwa kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano wa kuigwa katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Li Xueren)
Xi Jinping na viongozi wengine wa Chama cha Kikomunisti cha China na serikali wakitoa vyeti vya heshima kwa wajumbe wa watunukiwa kwenye mkutano wa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Shirikisho Kuu la Wafanyakazi la China na kusifu wafanyakazi wa kupigiwa mfano na watu wa mfano katika Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Aprili 28, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma