

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ahimiza kusukuma mbele kwa utaratibu maendeleo mazuri ya AI
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amehimiza juhudi za kusukuma mbele kwa utaratibu maendeleo mazuri ya teknolojia ya AI kwa mwelekeo wa manufaa, usalama na usawa wakati akiongoza mkutano wa wajumbe wote wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC siku ya Ijumaa.
Rais Xi amesisitiza kuwa, kwa kukabiliwa na maendeleo yenye mabadiliko ya haraka ya teknolojia za kizazi kipya cha AI, China itatumika vya kutosha nguvu yake bora ya mfumo mpya kwa kuhamasisha rasilimali za nchi nzima, kushikilia kujitegemea na kujiimarisha, kutoa kipaumbele kwa maendeleo yenye mwelekeo wa matumizi, na kuhimiza kwa utaratibu maendeleo mazuri ya teknolojia ya AI ya China kuelekea mwelekeo wa manufaa, usalama na usawa.
Zheng Nanning, profesa katika Chuo Kikuu cha Xi'an Jiaotong katika Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China, alitoa mhadhara kuhusu suala hili na kutoa mapendekezo. Wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC walisikiliza kwa makini mhadhara huo na kufanya majadiliano.
Akizungumza baada ya majadiliano hayo, Rais Xi amesema kuwa AI ikiwa teknolojia ya kimkakati inayoongoza raundi mpya ya mapinduzi ya kiteknolojia na mageuzi ya kiviwanda, imebadilisha kwa kina njia za uzalishaji na maisha ya binadamu. Amesema kuwa Kamati Kuu ya Chama inaweka umuhimu mkubwa sana kwenye maendeleo ya AI, na imefanya mpango wa jumla kwenye ngazi ya juu kuhusu utendaji wa pande mbalimbali, na kuimarisha juhudi za utekelezaji katika miaka ya hivi karibuni, na hivyo kuimarisha nguvu ya jumla ya maendeleo ya AI katika jumuishi na ya mfumo nchini China.
Na amesema kuwa bado kuna mapengo na mapungufu katika maeneo kama vile nadharia za kimsingi na teknolojia kuu za msingi, Rais Xi amehimiza kutambua mapungufu hayo na kuimarisha juhudi za kuendeleza kwa pande zote uvumbuzi wa sayansi-teknolojia, maendeleo ya viwanda na matumizi ya AI, kuboresha mifumo ya udhibiti na utaratibu wa AI, na kung'amua kithabiti juhudi zote katika maendeleo na usimamizi wa AI.
Amesisitiza kuwa mafanikio mapya lazima yapatikane katika nadharia, mbinu na zana za kimsingi ili kupata nguvu bora ya kuwa mwendeshaji wa kwanza na kupata uwezo wa ushindani katika AI.
Amehimiza juhudi za kuimarisha siku zote utafiti wa kimsingi na kujikita katika kuzishinda changamoto kuhusu teknolojia za msingi kama vile chipu za hali ya juu na programu ya msingi, na hivyo kujenga msingi wa programu na mfumo wa zana za AI ulio huru, unaoweza kudhibitiwa, na unaofanya kazi kiushirikiano.
Amesisitiza kuwa AI inaweza kutumika kama bidhaa nzuri ya umma duniani kote ambayo inanufaisha binadamu na ni muhimu kutekeleza kwa mapana ushirikiano wa kimataifa katika AI, kusaidia Nchi za Kusini kuimarisha ujengaji wao wa uwezo wa kiteknolojia, na kutoa mchango wa China kwa ajili ya kuziba pengo la mgawanyiko wa kimataifa wa AI.
“Jitihada zinapaswa kufanywa ili kuhimiza uwiano na uratibu wa mikakati ya maendeleo, sheria za usimamizi, na vigezo vya kiufundi kati ya pande zote, na kuunda mfumo wa usimamizi wa dunia na vigezo vyake vinavyokubaliwa kwa kina mapema iwezekanavyo,” Rais Xi amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma