Wanaanga wa China wa chombo cha Shenzhou-20 waingia kwenye kituo cha anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 25, 2025

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Aprili 25, 2025 ikionyesha picha ya pamoja ya wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-19 na Shenzhou-20. (Xinhua/Jin Liwang)

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Aprili 25, 2025 ikionyesha picha ya pamoja ya wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-19 na Shenzhou-20. (Xinhua/Jin Liwang)

BEIJING - Wanaanga watatu waliokuwa kwenye chombo cha anga ya juu cha China cha Shenzhou-20 ambacho kimerushwa jana Alhamisi jioni kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Jiuquan, kaskazini-magharibi mwa China wameingia kwenye kituo cha anga ya juu cha China na kukutana na wanaanga wengine watatu wa chombo cha Shenzhou-19 leo Ijumaa asubuhi, wakianza raundi mpya ya makabidhiano ya wanaanga ndani ya obiti.

Wanaanga hao wa chombo cha Shenzhou-19, ambao wamekuwa kwenye kituo cha anga ya juu cha China tangu walipopelekwa Oktoba 30, 2024, walifungua mlango majira ya saa 7:17 usiku wa manane (kwa saa za Beijing) na kuwasabahi na kuwakaribisha wanaanga hao wapya waliowasili, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limeeleza katika taarifa yake.

CMSA imesema kuwa, baada ya kukutana, wanaanga hao sita wakapiga picha pamoja, na hii ni mara ya sita kwa wanaanga wa vikundi tofauti wanajumuika pamoja kwenye anga ya juu katika historia ya anga ya juu ya China.

"Wataishi na kufanya kazi pamoja kwa siku tano hivi ili kukamilisha majukumu yaliyopangwa na kufanya kazi ya makabidhiano," CMSA imesema.

Wanaanga wa chombo cha Shenzhou-19 wamepangwa kurejea kwenye eneo la kutua la Dongfeng katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China Aprili 29.

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Anga cha Beijing Aprili 25, 2025 ikionyesha vikundi vya wanaanga wa vyombo vya anga ya juu vya Shenzhou-19 na Shenzhou-20 wakizungumza. (Xinhua/Jin Liwang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha