

Lugha Nyingine
Rais wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Azerbaijan
Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano asubuhi alifanya mazungumzo na mwenzake wa Azerbaijan Ilham Aliyev, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China ambapo viongozi hao wakuu wametangaza kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya nchi hizo mbili.
Rais Xi amesema, China inaiunga mkono Azerbaijan katika kulinda mamlaka, uhuru na ukamilifu wa eneo lake la taifa na kuendelea kufuata njia ya maendeleo inayolingana na hali yake ya kitaifa.
Rais Xi pia amesema, China inapenda kufanya kazi na Azerbaijan ili kudumisha mfumo wa kimataifa huku Umoja wa Mataifa ukiwa msingi wake na utaratibu wa kimataifa unaozingatia sheria za kimataifa, kulinda kithabiti haki na maslahi yake halali, na kutetea haki na usawa wa kimataifa.
Kwa upande wake, Bw. Aliyev amesema Azerbaijan inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kwamba Azerbaijan inapenda kufanya kazi na China ili kuimarisha zaidi ujenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, kupanua ushirikiano katika nyanja mbalimbali kama vile pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kuhimiza maendeleo zaidi ya uhusiano wa pande mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma