Rais Xi Jinping ahimiza umoja zaidi kati ya jeshi na raia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2025

Mkutano wa taifa ukifanyika ili kutuza miji na wilaya za kupigiwa  mfano katika kuhimiza uungaji mkono kati ya jeshi na serikali na kati ya jeshi na raia mjini Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 23, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Mkutano wa taifa ukifanyika ili kutuza miji na wilaya za kupigiwa mfano katika kuhimiza uungaji mkono kati ya jeshi na serikali na kati ya jeshi na raia mjini Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 23, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuwepo kwa umoja zaidi kati ya jeshi na serikali na kati ya jeshi na raia, akisisitiza haja ya kushikilia uongozi wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kwa pande zote, kusukuma mbele mageuzi na uvumbuzi, na kuboresha sera na mifumo husika.

Rais Xi, ambaye pia Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa maagizo hayo jana Jumatano kwenye mkutano wa taifa wa kutuza miji na wilaya za kupigiwa mfano katika kuhimiza uungaji mkono kati ya jeshi na serikali na kati ya jeshi na raia.

Katika maagizo hayo, Rais Xi ameelezea kuungana mkono kati ya sekta za jeshi na kiraia kama "jadi nzuri" na "faida ya kipekee ya kisiasa" kwa Chama, jeshi na raia.

Amezihimiza kamati za CPC na serikali katika ngazi mbalimbali kutilia maanani na kuunga mkono maendeleo na mageuzi ya jeshi, kushughulikia kwa makini taabu zinazowakabili maofisa na askari, na kuendeleza zaidi mazingira mazuri ya kijamii ambayo yanathamini ulinzi wa taifa, kuunga mkono jeshi, na kuheshimu wanajeshi.

Rais Xi amesisitiza kuwa jeshi linapaswa kujenga kithabiti ufahamu imara wa madhumuni yake ya kimsingi, kuunga mkono kikamilifu ujenzi na maendeleo ya maeneo husika, na kuchukua hatua madhubuti ili kuleta faida na kukuza ustawi kwa wananchi.

Ametoa wito wa kuongezwa ushirikiano kati ya jeshi na raia ili kuimarisha na kuendeleza umoja ulio imara kama mwamba kati ya jeshi na serikali, na kati ya jeshi na raia.

Akihutubia mkutano huo wa Jumatano, Waziri Mkuu wa China Li Qiang, ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, amesisitiza haja ya kutekeleza kithabiti maagizo hayo ya Rais Xi na kupata mafanikio mapya katika kuhimiza uungaji mkono wa pande zote kati ya jeshi na serikali na kati ya jeshi na raia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha