Xi ahutubia Mkutano wa Viongozi kuhusu Tabianchi na Mpito wa Haki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 24, 2025

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Viongozi  kuhusu Tabianchi na Mpito wa Haki, Aprili 23, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Viongozi kuhusu Tabianchi na Mpito wa Haki, Aprili 23, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Viongozi juu ya Tabianchi na Mpito wa Haki jana Jumatano akisema kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kusainiwa kwa Makubaliano ya Paris na maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) na huku mabadiliko ambayo hayakutokea duniani katika miaka mia moja iliyopita yakiendelea kwa kasi kubwa zaidi, binadamu wameingia katika njia panda mpya.

Amesema, ingawa kuna shauku kubwa ya nchi kubwa fulani kufanya utafutaji wa maslahi ya upande mmoja na kujilinda kibiashara inayoleta athari kubwa sana kwa kanuni za kimataifa na utaratibu wa kimataifa, historia, kama ilivyo wakati wote, itasonga mbele kupitia misukosuko na mabadiliko.

"Mradi tu tutaongeza kujiamini, kuwa na mshikamano na ushirikiano, tutashinda matatizo na kuhimiza usimamizi wa tabianchi duniani na mambo yote ya maendeleo ya dunia yaendelee kwa hatua madhubuti na kupata mafanikio siku za baadaye. " amesema.

Kuhusu hayo Rais Xi ametoa maoni yake kama yafuatayo: "Kwanza, lazima tushikilie mawasiliano na ushirikiano wa pande nyingi," kulinda kithabiti mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na utaratibu wa kimataifa uliowekwa kwenye msingi wa sheria za kimataifa, na kulinda kithabiti haki na usawa wa kimataifa.

Pili, ushirikiano wa kimataifa lazima uzidishwe zaidi, "Tunapaswa kupindukia utengano na migogoro kwa ufunguaji mlango na ujumuishi, kuongeza uvumbuzi wa kiteknolojia na mageuzi ya kiviwanda kupitia ushirikiano, na kuwezesha mzunguko huria wa teknolojia na bidhaa bora za kijani, ili ziweze kupatikana kwa bei rahisi na sifa nzuri kwa nchi zote, hasa zinazoendelea."

Aidha, China itazidisha kwa nguvu zaidi ushirikiano wa Kusini-Kusini na kuendelea kutoa msaada kwa iwezekanavyo kwa nchi zinazoendelea.

"Tatu, lazima tuharakishe mpito wa haki," mageuzi ya kijani lazima yaweke kipaumbele cha juu kwa umma, huku tukihimiza pia kuongeza ustawi wa watu na usimamizi wa tabianchi sanjari, na kufanya mpango wa jumla wa kutimiza malengo ya kulinda mazingira, kuendeleza uchumi, kuongeza nafasi za ajira na kupunguza umaskini.

Nne, lazima kuimarisha vitendo vinavyofanywa kwa kufuata hali halisi. "Pande zote zinapaswa kufanya juhudi kubwa zaidi kwa uwezo wao katika kupanga mipango yao ya utekelezaji iliyo ya kujichagia yenyewe kwa kila nchi kwenye msingi wa mpango wa jumla kuhusu maendeleo ya uchumi na mabadiliko ya muundo wa nishati," na kabla ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya taibianchi utakaofanyika Belem, Brazail, China itatangaza malengo yake ya kujichagia ya mwaka 2035 zinazohusisha nyanja zote za uchumi zikiwemo pamoja na gesi zote chafuzi.

Ameongeza kuwa, China inapenda kushirikiana na pande zote katika kubeba wajibu wa pamoja lakini wenye tofauti kwa kadiri ya uwezo wa kila nchi, na kuwa na mshikamano na ushirikiano, ili kujenga kwa pamoja dunia safi, ya kupendeza na yenye maendeleo endelevu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha