

Lugha Nyingine
Serikali ya Sudan yaidhinisha ujenzi wa kambi za ugavi za Umoja wa Mataifa magharibi mwa nchi hiyo
Serikali ya Sudan imetangaza kuwa, imekubali kujenga kambi za ugavi za Umoja wa Mataifa katika Jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa nchi hiyo.
Katika taarifa yake ya jana Jumatatu, Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan limesema, serikali imekubali ombi la Umoja wa Mataifa kuanzisha kambi hizo za ugavi kuzunguka mji wa El Fasher ili kuwezesha kazi za kibinadamu katika maeneo ya Mellit na Tawila.
Taarifa hiyo imesema, mwenyekiti wa Baraza hilo Abdel Fattah Al-Burhan aliwasiliana kwa simu jana Jumatatu na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura, Tom Fletcher, ambapo walijadili uwezekano wa kupeleka misaada mjini El Fasher huku wakikwepa vizuizi vilivyowekwa na askari wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) ama makundi mengine.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma