Hospitali za China na Msumbiji zafanya mashauriano ya matibabu mtandaoni juu ya magonjwa magumu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2025

Wataalamu wa timu ya madaktari wa China nchini Msumbiji na wakuu wa idara za upasuaji, mifupa na upasuaji wa neva za fahamu upande wa Msumbiji  wakishiriki kwenye mashauriano ya kimataifa ya matibabu mtandaoni kati ya Hospitali ya Huaxi  ya Chuo Kikuu cha Sichuan na Hospitali Kuu ya Maputo ya  Msumbiji, Aprili 21, 2025. (Xinhua/Liu Jie)

MAPUTO – Mashauriano ya kimataifa ya matibabu yenye mafanikio yamefanyika jana Jumatatu kati ya Hospitali ya Huaxi ya Chuo Kikuu cha Sichuan cha China na Hospitali Kuu ya Maputo ya Msumbiji, ikiwa ni sehemu ya kazi ya ushirikiano wa kimatibabu inayoendelea kufanywa na Timu ya 25 ya Madaktari wa China nchini humo.

Mashauriano hayo yamewakutanisha pamoja wataalamu wa upasuaji, mifupa, upasuaji wa neva za fahamu na matibabu ya dharura kutoka hospitali zote mbili. Washiriki ni pamoja na wataalam wa China kutoka Hospitali ya Huaxi ya China, wataalam wa timu ya madaktari wa China nchini Msumbiji, na wakuu wa idara za upasuaji, mifupa na upasuaji wa neva kwa upande wa Msumbiji.

Matibabu ya magonjwa ya wagonjwa wanne yalipitiwa kwenye mashauriano hayo, na majadiliano zaidi ni kuhusu upimaji na uthibitishaji wa magonjwa, mikakati ya matibabu, changamoto za upasuaji, na mapungufu katika rasilimali za matibabu.

"Hii ni fursa muhimu sana kwetu," amesema Barnabe Antonio Deuasse, mkurugenzi wa idara ya mifupa ya Hospitali Kuu ya Maputo, akiongeza kuwa mashauriano hayo si kama tu yanatoa fursa ya kupata ujuzi wa matibabu ya zama za hivi sasa, bali pia yametoa mipango ya utekelezaji ya kudhibiti magonjwa magumu katika hali yenye upungufu wa rasilimali.

"Inatia moyo kujua tunaweza kutegemea maoni ya pili na uungaji mkono wa wataalamu tunapokabiliwa na hali ngumu. Daima tuko tayari kufanya ushirikiano na kutoa mifano ya magonjwa magumu kwenye majadiliano zaidi... Tunatumai kutakuwa na majadiliano zaidi katika siku zijazo," amesema Barnabe.

Mashauriano hayo yamehitimishwa kwa maelezo ya Atilio Morais, mkuu wa upasuaji katika Hospitali Kuu ya Maputo, ambaye amesisitiza thamani ya mashauriano hayo katika kuongeza utaalamu wa kimatibabu na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika matibabu. 

Wataalamu wa timu ya madaktari wa China nchini Msumbiji na wakuu wa idara za upasuaji, mifupa na upasuaji wa neva za fahamu upande wa Msumbiji wakihudhuria wakishiriki kwenye mashauriano ya kimataifa ya matibabu mtandaoni kati ya Hospitali ya Huaxi ya Chuo Kikuu cha Sichuan cha China na Hospitali Kuu ya Maputo ya Msumbiji, Aprili 21, 2025. (Xinhua/Liu Jie)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha