Waziri wa Mambo ya Nje wa China afanya mazungumzo na mwenzake wa Indonesia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 22, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),Wang Yi akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Sugiono mjini Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 21, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)

BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amefanya mazungumzo na mwenzake wa Indonesia Sugiono mjini Beijing jana Jumatatu akisema kuwa China na Indonesia zimepata maafikiano muhimu kuhusu kujenga jumuiya ya China na Indonesia yenye mustakabali wa pamoja ambayo ina ushawishi wa kikanda na kimataifa.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kuwa nchi hizo mbili pia zimefikia maafikiano muhimu ya kuboresha muundo wa ushirikiano kutoka "nguzo nne" za kisiasa, kiuchumi, mabadilishano kati ya watu na watu, na bahari, hadi ushirikiano katika "nguzo tano" kwa kuongeza usalama kama nguzo ya tano ya ushirikiano, ikifungua matarajio mapana ya ushirikiano kati ya China na Indonesia.

Amesema pande hizo mbili zinapaswa kuimarisha ushirikiano katika kuhimiza ushirikiano wa kiwango cha juu, kushikilia biashara huria, kuendeleza viwanda vinavyoibukia, na kupanua ushirikiano unaojikita katika kuboresha maisha ya watu.

Akibainisha kuwa mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa Umoja wa Mataifa na maadhimisho ya miaka 70 tangu kufanyika Mkutano wa Bandung, Wang amesema kuwa katikati ya vita vya kibiashara duniani vinavyochochewa na Marekani na misukosuko inayoathiri utandawazi wa kiuchumi, China na Indonesia, kama walinzi wa utandawazi wa kiuchumi na uhuria wa kibiashara, zinapaswa kuchukua jitihada ya kihistoria kuongeza hali ya kuaminiana na ushirikiano.

Wang amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kushirikiana kuhimiza Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani na Moyo wa Bandung, kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi huku WTO ikiwa katika msingi wake, kulinda haki na usawa wa kimataifa, na kutuma ishara ya umoja na uwazi kwa dunia, ikionyesha zaidi ushawishi wa kikanda na kimataifa wa uhusiano kati ya China na Indonesia.

Akisema kuwa China ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara na chanzo kikuu cha uwekezaji wa kigeni wa Indonesia, Sugiono amesema Indonesia siku zote imekuwa ikiichukulia China kama mojawapo ya washirika wake muhimu, na kwamba uhusiano wa pande mbili umedumisha kasi kubwa kwa miaka mingi.

Ameongeza kuwa Indonesia inatarajia kuimarisha mawasiliano na China katika ngazi zote, na kupanua ushirikiano wa kivitendo katika biashara, uwekezaji, kilimo, uvuvi, huduma za afya, nishati safi, uvumbuzi wa kisayansi vilevile mawasiliano kati watu na ya kitamaduni.

Siku hiyo hiyo, tafrija ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na miaka 70 tangu kufanyika Mkutano wa Bandung imefanyika mjini Beijing.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Wang Yi, Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun, Sugiono na Waziri wa Ulinzi wa Indonesia Sjafrie Sjamsoeddin.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),Wang Yi akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Sugiono mjini Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 21, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),Wang Yi akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Sugiono mjini Beijing, mji mkuu wa China, Aprili 21, 2025. (Xinhua/Zhang Ling)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC),Wang Yi, Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun, Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Sugiono na Waziri wa Ulinzi wa Indonesia Sjafrie Sjamsoeddin wakihudhuria tafrija ya kuadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na maadhimisho ya miaka 70 tangu kufanyika Mkutano wa Bamdung mjini Beijing, Mji Mkuu wa China, Aprili 2, 2019. (Xinhua/Yue Yuewei)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha