

Lugha Nyingine
Rais Xi Jinping ampongeza Nguema kwa kuchaguliwa kuwa rais wa Gabon
BEIJING - Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za pongezi kwa Brice Clotaire Oligui Nguema kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Gabon, akisema kuwa China na Gabon zina urafiki wa jadi, na katika miaka ya hivi karibuni, kuaminiana kisiasa kati ya nchi hizo mbili kumeendelea kuzidishwa, na ushirikiano katika sekta mbalimbali umepata matokeo mengi mazuri. “Nchi hizi mbili zimekuwa zikiungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya msingi na masuala makubwa yanajaliwa na kila upande,” ameongeza katika salamu hizo za pongezi zilizotumwa Jumamosi.
Rais Xi pia amesema kwamba anaweka umuhimu mkubwa sana kwenye maendeleo ya uhusiano kati ya China na Gabon na anapenda kushirikiana na Rais mteule Nguema katika kuchukua utekelezaji matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kama fursa ya kuhimiza ukuaji halisi wa kina wa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili, ili kunufaisha vizuri watu wao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma