

Lugha Nyingine
Maoni: “China inapeleka Upendo badala ya kutoza kodi”
Hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya kiserikali katika nchi tatu za Vietnam, Malaysia na Cambodia kutokana na mwaliko, ambapo alikaribishwa kwa furaha na serikali na watu wa nchi hizo, hali ambayo ilimfanya mtu mmoja wa nchi ya nje aandike kwenye mtandao kuwa, “China inapenda nchi zake jirani. China inapeleka upendo badala ya kutoza kodi.”
Maneno haya ni uelewa kweli kuhusu wazo la China la upendo, udhati, kunufaishana na ujumuishaji katika mambo ya diplomasia ya ujirani, zaidi yanasifu kwa dhati China kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya nchi jirani yenye mustakabali wa pamoja.
Rais Xi mwenyewe amefanya ziara katika nchi 27 jirani za China, na ziara yake ya kwanza baada ya mkutano mkuu wa 18, 19, 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China zote zilikuwa katika nchi jirani. China inafanya juhudi za kushirikiana na nchi jirani, ikianzisha njia pana ya ujirani mwema na ushirikiano wa kunufaishana kwa pande zote.
Kutafuta ustawi kwa pamoja kutokana na maendeleo. China na nchi 25 jirani zimesaini makubaliano ya kujenga pamoja “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na China imekuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara kwa nchi 18 kati ya nchi hizo; Biashara kati ya China na Umoja wa nchi za Asia ya Kusini Mashariki (ASEAN) imefikia Yuan trilioni 6.99 mwaka 2024, ikichukua 15.9% ya thamani ya jumla ya biashara ya China na nchi za nje.
Kuzidisha urafiki wa kizazi hadi kizazi kutokana na ustaarabu. Mawasiliano ya kiutamaduni kati ya China na Vietnam yanaendelea kwa kina siku hadi siku. Hivi sasa takriban wanafunzi 240,000 wa Vietnam wanasoma nchini China; Karakana za Luban zimekita mizizi katika nchi nyingi jirani za China, zikiwa “vituo vya elimu” vinavyosifiwa sana kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.
Kulinda maskani ya pamoja kutokana na kubeba wajibu. China na nchi 17 jirani zake zimefikia maoni mamoja ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja; Katika kukabiliana na changamoto dhidi ya usalama usio wa kijadi, kufanya ushirikiano katika utekelezaji wa sheria wa Lancang-Mekong kumegunduliwa kwa matukio mengi ya aina mbalimbali ya uhalifu wa jinai wa kuvuka mipaka; Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) imeongeza nchi wanachama zaidi, ikionesha nia na matumaini ya watu ya kulinda amani na kupata maendeleo kwa pamoja.
Hivi sasa mabadiliko yanaendelea kwa kasi duniani, na hali ya kimataifa imekabiliwa na misukosuko. Wakati fimbo kubwa ya kodi inapopiga matumaini ya maendeleo ya nchi maskini na dhaifu, China inachagua sera ya kutotoza kodi na kufungua mlango wake kwa mazao ya kilimo ya nchi 33; Wakati hali ya kujilinda kibiashara imejenga “uzio mrefu wa ua mdogo”, treni za China-Ulaya zimeunganisha miji 227 katika nchi 25 za Ulaya na miji zaidi ya mia moja katika nchi 11 za Asia, zikiwezesha bidhaa za nchi nyingi kunufaika pamoja na soko kubwa la China. China haifuati njia potofu ya “nchi yenye nguvu lazima kuwa nchi yenye umwamba, na nchi kubwa inadhulumu nchi ndogo”, badala yake inaleta manufaa kwa dunia kutokana na maendeleo yake, na kupata heshima kwa kubeba wajibu wake.
“China inapeleka upendo badala ya kutoza kodi.” Maneno hayo rahisi yameonesha China inanyanyua bendera ya jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, na imeleta nuru kwa matumaini ya ushirikiano kwa kubeba majukumu na wajibu wake wa nchi kubwa katika dunia inayokabiliwa na mabadiliko na misukosuko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma