Jukwaa la nchini Kenya latoa wito wa suluhu endelevu kwa changamoto za uhamiaji za Somalia

(CRI Online) April 21, 2025

Watunga sera, wataalamu wa uhamiaji na wadau wa kikanda katika jukwaa la Mkutano wa Mwaka wa Uhamiaji liliofanyika jana Jumapili katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wametoa wito wa suluhu za muda mrefu na endelevu ili kukabiliana na vyanzo vya wakimbizi wa ndani na wahamiaji katika Pembe ya Afrika.

Ukiwa umefanyika chini ya kaulimbiu ya “Kupata Suluhu Endelevu kwa Uhamiaji nchini Somalia,” mkutano huo umewakutanisha wawakilishi kutoka serikali, mashirika ya kikanda, Umoja wa Mataifa, mashirika ya kiraia, na taasisi za elimu ili kujadili vyanzo mbalimbali vya uhamiaji nchini Somalia, ikiwemo mapigano, umaskini, mabadiliko ya tabianchi, na mifumo dhaifu ya uongozi.

Balozi wa Somalia nchini Kenya, Jabril Ibrahim Abdulle amesisitiza haja ya amani ya kudumu, maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na ushirikiano wa kuvuka mpaka ili kudhibiti uhamiaji holela na wakimbizi wa ndani nchini Somalia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha