Makao Makuu ya Shirika la Anga ya Juu la Afrika yazinduliwa nchini Misri

(CRI Online) April 21, 2025

Misri imezindua makao makuu ya Shirika la Anga ya Juu la Afrika (AfSA) katika mji wa Anga ya Juu ulioko Cairo, mji mkuu wa nchi hiyo.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa makao makuu hayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Badr Abdelatty amesema Misri imefanya juhudi kubwa kuanzisha shirika hilo, ambalo linajumuisha dira ya “Afrika Tunayoitaka” iliyoorodheshwa kwenye Ajenda ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2063.

Amesisitiza kuwa shirika hilo litatumika kama jukwaa la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika katika matumizi ya amani ya anga ya juu, kubadilishana utaalamu, kujenga uwezo, na kuunganisha nafasi ya Afrika katika majukwaa ya kimataifa, hususan mfumo wa Umoja wa Mataifa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha