

Lugha Nyingine
Idadi ya vifo kwa mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na wafugaji katikati ya Nigeria yafikia 56
(CRI Online) April 21, 2025
Gavana wa Jimbo la Benue, katikati mwa Nigeria Bw. Hyacinth Alia amesema, mashambulizi ratibiwa yaliyofanywa watu wanaoshukiwa kuwa wafugaji wenye silaha katika jimbo hilo, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 56 hadi sasa, huku vyombo vya usalama na watu wa kujitolea jimboni humo wakiendelea kutafuta kwenye vichaka vilivyo karibu kupata miili zaidi.
Akizungumza na waandishi juzi Jumamosi, Bw. Alia amelalamikia mashambulizi hayo mabaya, baada ya tathmini ya eneo la tukio kuonyesha kwamba wakazi wa eneo hilo wameshambuliwa kwa makusudi mwanzoni mwa msimu wa kilimo, ili kuwazuia kulima.
Ametoa wito wa kuchukua hatua za haraka ili kukabiliana na hali hiyo mbaya na kukomesha mashambulizi yanayoendelea kuzikumba jamii za jimbo hilo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma