Israel kuendeleza operesheni za kijeshi mjini Gaza hadi malengo ya mapigano yatakapotimia

(CRI Online) April 21, 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema mwishoni mwa wiki kuwa Israel haitasitisha operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza hadi malengo yake ya kivita yatakapofikiwa.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi kwa njia ya video, Bw. Netanyahu amesema, Kundi la Hamas halikutimiza ahadi yake ya kuachilia huru baadhi ya mateka likiitaka Israel ikomeshe vita na kuondoa wanajeshi wake katika Ukanda wa Gaza.

Amesisitiza kuwa Jeshi la Israel halitasitisha operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza hadi pale kundi la Hamas litakapotokomezwa, mateka wote katika Ukanda wa Gaza kuachiliwa, na kuhakikishwa kuwa Ukanda wa Gaza si tishio tena kwa Israel.

Kwa mujibu wa Netanyahu, bado kuna Waisraeli 24 wanaoshikilia mateka katika Ukanda wa Gaza huku wengine 35 wakiwa wamethibitishwa kuuawa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha