Uzuri wa Vipindi vya Kalenda ya Kilimo ya China: Mvua ya Nafaka

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 20, 2025

Uzuri wa Vipindi vya Kalenda ya Kilimo ya China: Mvua ya Nafaka

Habari zenu! Mpenda kusafiri Sisi hapa! Leo ni Guyu, au Mvua ya Nafaka, kipindi cha sita katika kalenda ya kilimo ya China yenye vipindi 24 na cha mwisho katika majira ya mchipuko. Nimefika kwenye Mlima Wuyi wenye mandhari ya kuvutia sana, unaopatikana Mkoa wa Fujian, kusini-mashariki mwa China. Nifuate na furahia uzuri wa mandhari haya!

Kipindi hiki cha Mvua ya Nafaka kilipata jina lake kutoka kwenye msemo "Mvua huleta ukuaji wa mamia ya nafaka." Baridi inayojitokezatokeza ya majira ya mchipuko hufifia, mvua inayonyesha hulowesha dunia, na vitu vyote hukua kwa kustawi.

Kipindi hiki cha Mvua ya Nafaka ni muhimu kwa kuchuma na kuonja chai. Chai iliyochumwa na kusindikwa wakati wa kipindi hiki mara nyingi huitwa "Chai ya Mvua ya Nafaka" au "Chai ya Pili ya Majira ya Mchipuko," na inatambulika kuwa bora zaidi katika mwaka. Kiini cha majira mazima ya mchipuko hugeuzwa kimiminika kwenye kikombe cha radha ya chai.

Unajua nini? Mlima Wuyi si tu ni mahali pa kuzaliwa kwa oolong na chai nyeusi, lakini kijiji cha Xiamei, ambapo ninasimama sasa, pia ni mahali pa kuanzia kwa njia ya kale ya chai ya karne ya 17. Kutoka hapa, harufu nzuri ya chai ilisafiri kuelekea kote Eurasia, ikiacha athari ya kudumu kwenye utamaduni wa chai duniani kote.

Simulizi iliyopo ni kwamba, kipindi hiki cha Mvua ya Nafaka huashiria siku ambayo Cang Jie, mvumbuzi wa herufi za Kichina, alimaliza kazi yake. Tangu nyakati za zamani, kimekuwa ni wakati wa kumheshimu kwa kazi yake hiyo. Ili kuadhimisha michango yake, Idara ya Habari kwa Umma ya Umoja wa Mataifa imeiteua "Siku ya Lugha ya Kichina ya Umoja wa Mataifa" kufanyika wakati wa kipindi cha Mvua ya Nafaka kila mwaka.

"Huku kipindi cha Mvua ya Nafaka kikiwadia, mwanga wa majira ya mchipuko humulika; milima na mito hugeuka kijani." Majira ya mchipuko yanapotokomea na majira ya joto kuwasili, hebu tufurahie kumbukumbu za majira ya mchipuko mioyoni mwetu na tukaribishe kuwasili kwa majira ya joto yenye hali motomoto.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha