

Lugha Nyingine
Kenya yaandaa kongamano la ushirikiano kati ya China na Afrika kuhusu suluhu za kuvuna maji ya mvua
Kongamano la ngazi ya juu lenye lengo la kukuza ushirikiano kati ya China na Afrika katika usimamizi wa rasilimali za maji lilifanyika mjini Nairobi, Kenya, likijikita katika kutoa utaalamu wa China ili kusaidia usambazaji endelevu wa maji katika bara zima.
Kongamano hilo linalojulikana kama Warsha ya Gansu iliyofanyika kwa siku moja liliwaleta pamoja wataalamu, watafiti, na maafisa wa serikali kutoka China na nchi za Afrika ili kubadilishana mbinu bora, kuhimiza mazungumzo, na kutafuta suluhu za kivitendo kwa maeneo yenye uhaba wa maji barani Afrika.
Wawakilishi kutoka Chuo cha Uhifadhi wa Maji cha Gansu walieleza mifano ya kufanikiwa kuvuna maji ya mvua na mifumo midogo ya umwagiliaji iliyotekelezwa nchini China.
Akielezea matumizi mabaya ya rasilimali za maji kwenye kongamano hilo, ofisa mkuu mtendaji wa Taasisi ya Maji ya Kenya inayomilikiwa na serikali Solomon Leiro Letangule amesema kati ya mita za ujazo bilioni 354 za maji ya mvua zinazopatikana kila mwaka nchini Kenya, ni mita za ujazo milioni 55.4 tu zinavunwa. Ameongeza kuwa Kenya ina nia ya kuendeleza ushirikiano na China, kwa sababu inahitaji wataalamu waliobobea kutoa huduma za kiufundi, ushauri na mafunzo ili kuimarisha juhudi zake za kuhifadhi maji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma