Rais wa Kenya kufanya ziara nchini China

(CRI Online) April 18, 2025

Kufuatia mwaliko wa rais Xi Jinping wa China, Rais William Ruto wa Kenya atafanya ziara ya kiserikali nchini China kuanzia Aprili 22 hadi 26.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lin Jian amebainisha kuwa urafiki kati ya China na Kenya umeanzia kwenye Njia ya Hariri ya kale ya Baharini, na katika zama mpya, nchi hizo mbili zimeanzisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati wa kina, unaojumuisha mawasiliano ya mara kwa mara ya ngazi ya juu, kuendelea kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, matunda mazuri yaliyopatikana kwenye ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na ushirikiano wa karibu katika masuala ya kikanda na kimataifa.

Katika ziara hiyo, Rais Xi atafanya mazungumzo na mwenzake Ruto, ambapo pia Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma Zhao Leji pia watakutana naye mtawalia.

Msemaji Lin amesema China ina imani kwamba ziara hii itachangia kuimarisha uhusiano kati ya China na Kenya, kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kujenga jumuiya ya hali zote yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya, na kuendeleza umoja na ushirikiano kati ya mataifa ya Kusini mwa Dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha