

Lugha Nyingine
China yaendelea kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara na mchangiaji muhimu wa maendeleo kwa Afrika
Maafisa wa China na Umoja wa Afrika wamesema ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika unazidi kushika kasi, ambapo thamani ya biashara katika mwaka 2024 imeongezeka hadi dola za kimarekani bilioni 295, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6 kuliko mwaka uliopita.
Akiongea kwenye mkutano wa sera kuhusu uchumi na ushirikiano wa kibiashara wa China na Afrika, ulioandaliwa kwa pamoja na Ujumbe wa China na Chama cha Wafanyakazi wa AU mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia, Mkuu wa Ujumbe wa China katika AU Hu Changchun alisema China imekuwa mshirika mkuu wa kibiashara barani Afrika kwa miaka 15 mfululizo. Takriban nusu ya nchi za Afrika zimesajili ongezeko la tarakimu mbili katika viwango vya biashara na China mwaka jana.
Mkutano huo unalenga kuongeza uelewa wa pamoja na kutafuta fursa zaidi za maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika. Akiangazia ushirikiano wa muda mrefu wa China na Afrika, Bw. Hu amesema sera za kurahisisha biashara chini ya Jukwaa la Mfumo wa Ushirikiano kati ya China na Afrika na Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” zimehamasisha makampuni mengi zaidi ya China kwenda Afrika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma