Uhusiano wa Xi Jinping na Chai ya Fujian

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2025

China ni maskani ya chai. Fujian ni mkoa mkubwa kwa uzalishaji chai. Fujian ina hekta zaidi ya laki 2 za mashamba ya chai. Inazalisha aina mbalimbali za chai: nyeusi, nyeupe, kijani na ya oolong.

Xi Jinping ambaye aliwahi kufanya kazi mkoani Fujian kwa zaidi ya miaka 17, ana “uhusiano wa chai” wa kina na Fujian. Aprili 2002, Xi Jinping, wakati huo akiwa Mkuu wa Mkoa wa Fujian, alimtembelea mwanakijiji Yan Jinyou nyumbani, akamtia moyo kuchagua njia ya maendeleo inayomfaa na yenye uhakika wa mafanikio. Alimshauri ajikite katika uzalishaji wa chai na akamtakia mafanikio ya mara kwa mara.

Mwaka 2017, viongozi wa nchi za BRICS walikutana Xiamen. Zawadi ya kitaifa aliyoitoa Rais Xi Jinping ilikuwa boksi la zawadi la aina mbalimbali za chai wakilishi maarufu na bora kutoka Fujian.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha