Rais Xi asema kujenga jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja ni chaguo la historia na watu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 18, 2025

Rais wa China Xi Jinping akikutana na  Mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Cambodia ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Seneti Samdech Techo Hun Sen katika Ikulu ya Amani mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Cambodia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Seneti Samdech Techo Hun Sen katika Ikulu ya Amani mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Xie Huanchi)

PHNOM PENH - Rais wa China Xi Jinping jana Alhamisi mjini Phnom Penh alipokutana na Mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Cambodia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Seneti Samdech Techo Hun Sen, alisema kwamba, kujenga jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja ni chaguo la historia na watu.

Amesema, China na Cambodia si kama tu ni majirani wa kirafiki bali pia ni marafiki imara kama chuma, na nchi zote mbili kwa sasa ziko katika kipindi muhimu cha maendeleo ya nchi.

Rais Xi amesema kuwa pande hizo mbili zinapaswa kutilia maanani zaidi ustawi wa watu wao na maendeleo ya binadamu, kujitahidi kuweka mfano kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja katika lengo la kuendelea na juhudi zao za ujenzi wa mambo ya kisasa, na kushikana mikono ili kuwa nguvu za amani, utulivu na maendeleo katika dunia inayopitia mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita.

Rais Xi amesema, "China inaamini kuwa barabara ya Cambodia kwa maendeleo na ustawishaji wa taifa itakuwa pana na pana zaidi, na kama ilivyofanya wakati wote, China itakiunga mkono Chama cha Umma cha Cambodia katika kuongoza watu wa Cambodia kudumisha utulivu na maendeleo ya uchumi ya nchi, " na inaunga mkono Cambodia kuonesha kazi yake muhimu zaidi katika majukwaa ya kikanda na kimataifa.

Rais huyo wa China amesema, pande hizo mbili zinapaswa kutumia vyema utaratibu mpya ulioanzishwa wa "2+2" wa mazungumzo ya kimkakati kati ya mawaziri wa mambo ya nje na mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili ili kuimarisha uratibu wa kimkakati.

Rais Xi amesema, hatua za upande mmoja na umwamba havitaungwa mkono na watu, historia imeonyesha mwelekeo usiozuilika kuelekea dunia ya ncha nyingi, utandawazi wa kiuchumi, na ustaarabu mbalimbali na hakuna nchi inayotaka kurudi kwenye hali ya kutengana.

Vita vya kibiashara vinadhoofisha mfumo wa biashara wa pande nyingi na kuvuruga utaratibu wa uchumi wa dunia, Rais Xi amesema, akihimiza nchi zote kuwa wamoja na kushika kithabiti hatamu za usalama na maendeleo ya nchi mikononi mwao, kushikilia kuheshimiana, kutafuta ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote na kupata maendeleo kwa pamoja, na kufanya juhudi za pamoja za kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Kwa upande wake, Hun Sen amesema ziara hiyo ya Rais Xi ina umuhimu mkubwa kwa Cambodia.

Hun Sen amesema kuwa China ni muungaji mkono thabiti na mshirika wa kutegemewa zaidi wa Cambodia, uungaji mkono wa China umetoa mchango muhimu kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Cambodia na kuboresha maisha ya watu, Cambodia inatoa shukrani zake za dhati kwa hayo yote.

Akisisitiza kuwa vita vya kibiashara na ushuru vimedhoofisha maslahi halali ya nchi zote na kusababisha msukosuko katika hali ya kimataifa, Hun Sen amesema Cambodia inapenda kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa kiusalama na China na kupanua biashara ya pande mbili.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Cambodia ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Seneti Samdech Techo Hun Sen katika Ikulu ya Amani mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Mwenyekiti wa Chama cha Umma cha Cambodia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Seneti Samdech Techo Hun Sen katika Ikulu ya Amani mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha