

Lugha Nyingine
China na Cambodia zakubaliana kujenga jumuiya ya majira yote yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya
Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet katika Ikulu ya Amani mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Liu Weibing)
PHNOM PENH - Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet wamekubaliana jana Alhamisi kujenga jumuiya ya China na Cambodia ya majira yote yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na kuamua mwaka 2025 kuwa Mwaka wa Utalii kati ya China na Cambodia.
Rais Xi amesema urafiki wa kithabiti ulio kama chuma kati ya China na Cambodia una historia ndefu, msingi imara wa kisiasa na nguvu endeshi ya ndani, na haijalishi hali ya kimataifa inabadilika kwa namna gani, nchi hizo mbili daima zimekuwa mstari wa mbele katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Rais Xi amesema kuwa hivi sasa, mabadiliko ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita yanaongezeka kwa kasi, kuzidisha ujenzi wa jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja kunalingana kabisa na maslahi ya kimsingi ya watu wa pande hizo mbili.
Ameongeza kuwa, "China, kama ilivyofanya siku zote, itaiunga mkono Cambodia katika kufuata njia ya maendeleo inayofuata hali halisi ya nchi yake, kuunga mkono serikali ya Cambodia kutawala nchi bila vizuizi, na kuunga mkono Cambodia kuonesha kazi yake muhimu zaidi katika masuala ya kimataifa na kikanda".
Rais Xi ametoa wito kwa pande zote mbili kuchukua ujenzi wa jumuiya ya majira yote ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya kama mwanzo mpya, kuendelea kufanya juhudi kubwa zaidi za kutekeleza mpango mpya wa utendaji wa kujenga jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja, kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kuharakisha utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia.
Pia amehimiza pande hizo mbili kuzidisha hali ya kuaminiana kisiasa kwenye ngazi ya juu zaidi, kupanua ushirikiano wa kunufaishana wa kiwango cha juu, kuongeza uhakikishaji wa usalama wa ngazi ya juu, kuongeza zaidi mawasiliano ya kitamaduni, na kuimarisha uratibu wa kimkakati kwa vigezo vya juu zaidi, ili kuleta manufaa zaidi kwa watu wa pande hizo mbili.
Rais Xi amesema, Upande wa China unapenda kunufaika na fursa na kutafuta maendeleo pamoja na Cambodia.
Ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuchukua hatua yenye nguvu kubwa na ufanisi zaidi za kukabiliana na uchezaji kamari mtandaoni na ulaghai wa mawasiliano ya simu, na kudumisha utulivu wa kijamii na utaratibu wa kawaida wa mawasiliano kati ya nchi za kikanda.
Amesema China na Cambodia, zikiwa nguvu muhimu za Nchi za Kusini, zinapaswa kushikilia maadili ya pamoja ya amani, mshikamano na ushirikiano, kupinga vitendo vya umwamba vya upande mmoja, kutekeleza ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kupinga kithabiti misuguano ya kambi, kuimarisha uratibu na ushirikiano ndani ya mifumo ya Ushirikiano wa ASEAN na Lancang-Mekong, na kulinda kwa pamoja amani ya kikanda iliyopatikana kwa juhudi kubwa, ili kuchangia kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Kwa upande wake, Hun Manet amesema Cambodia na China zimekuwa zikiheshimiana kwa muda mrefu na kutendeana kwa usawa, na China ni rafiki wa kutegemewa na wa kuaminika wa Cambodia.
Amesema ziara hiyo ya Rais Xi ni yenye umuhimu mkubwa, ambayo itazidisha ipasavyo hali ya kuaminiana kisiasa kati ya nchi hizo mbili na kuhimiza kwa nguvu ujenzi wa jumuiya ya Cambodia na China yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Baada ya mkutano huo, viongozi hao wa nchi hizo mbili walishuhudia makabidhiano ya zaidi ya nyaraka 30 za ushirikiano wa pande mbili kuhusu ushirikiano wa minyororo ya uzalishaji na usambazaji bidhaa, teknolojia za kisasa, msaada wa maendeleo, ukaguzi wa forodha na karantini, vilevile ushirikiano katika sekta za afya na vyombo vya habari.
Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Cambodia Hun Manet katika Ikulu ya Amani mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Ding Haitao)
Rais Xi Jinping wa China na Waziri Mkuu wa Cambodia, Hun Manet kwa pamoja wakishuhudia makabidhiano ya nyaraka za ushirikiano wa pande mbili baada ya mazungumzo yao mjini Phnom Penh, Cambodia, Aprili 17, 2025. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma