

Lugha Nyingine
Wanafunzi wanne washinda Shindano la Daraja la Lugha ya Kichina nchini Tanzania
Wanafunzi wanne wa vyuo vikuu vya Tanzania wameibuka washindi wa Shindano la 24 la Darala la Lugha ya Kichina upande wa Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mashindano ya Wanafunzi wa Vyuo vya Kigeni duniani kote.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Confucius ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yalikuwa na washiriki 16 kutoka taasisi hiyo, Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Ndaki ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Kituo cha Uhusiano wa Nje cha Dk. Salim Ahmed Salim.
Mwanafunzi kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kulthum Athuman Maftah amechaguliwa kuwa mshindi wa jumla, na atashiriki fainali za kimataifa mwezi Mei.
Mashindano hayo yamepima ujuzi wa washiriki wa lugha ya Kichina katika kuzungumza, kusoma, kuandika na kusikiliza. Pia yamejumuisha maonyesho ya kiutamaduni kama vile kuimba, kughani mashairi, onyesho la kungfu, na ufahamu wa mambo kuhusu China.
Kaimu naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rose Upor amepongeza Taasisi za Confucius kwa kuimarisha mabadilishano ya kiutamaduni na kielimu kati ya China na Afrika, akisisitiza kwamba kujifunza lugha ya Kichina kutaongeza matarajio ya ajira na kuna wazungumzaji zaidi ya laki mbili wa lugha ya Kichina na kampuni zaidi ya 500 za Kichina nchini Tanzania.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma