Rais wa Kenya aapa kuimarisha jeshi ili kukabiliana vitisho vya usalama

(CRI Online) April 17, 2025

Rais wa Kenya William Ruto Jumatano amesisitiza tena azma ya utawala wake katika kuimarisha jeshi la nchi hiyo ili kukabiliana na vitisho vya usalama.

Akiongea kwenye gwaride la kuanza mafunzo ya ukadeti katika Chuo cha Jeshi cha Kenya katika Kaunti ya Nakuru, Rais Ruto amesema serikali yake inaboresha vikosi vya ulinzi vya Kenya (KDF) na kufanya mafunzo yao yaende sambamba na mazingira yanayoibuka haraka ya usalama kutokana na vitisho visivyo vya kawaida, vita vya kimtandao, na changamoto za kimataifa.

Maafisa wapya wa kadeti walioanza mafunzo ni pamoja na askari kutoka Burkina Faso, Msumbiji, Rwanda, Sierra Leone, Tanzania, na Uganda. Kikosi hicho pia kina wahitimu wa kwanza kupata shahada ya kwanza katika masomo ya ulinzi na usalama katika Chuo Kikuu cha Ulinzi cha Kenya.

Aidha Rais Ruto amesisitiza umuhimu wa jukumu la pamoja katika kuhakikisha usalama wa taifa, akibainisha kuwa hakuna nguvu ya jeshi moja pekee inayoweza kuhakikisha usalama wa nchi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha