

Lugha Nyingine
Kiwango cha umaskini cha Rwanda chapungua hadi asilimia 27.4
Matokeo ya Utafiti Jumuishi wa saba wa Hali ya Maisha ya Kaya, yaliyotangazwa Jumatano na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Rwanda (NISR) mjini Kigali, yanaonesha kuwa kiwango cha umaskini nchini humo kimeshuka sana kutoka asilimia 39.8 cha mwaka 2017 hadi asilimia 27.4 mwaka 2024, ikiashiria kupungua kwa asilimia 12.4 katika miaka saba iliyopita.
Utafiti huo uliofanywa kati ya Oktoba 2023 na Oktoba 2024, unaonesha kwamba mikoa yote ya nchi hiyo imepunguza umaskini.
Huku viwango vya mikoa vikiendelea kutobadilika, na Jiji la Kigali kuripoti viwango vya chini vya umaskini, na majimbo ya kusini na magharibi yakiwa na viwango vya juu zaidi, sehemu ya Wanyarwanda wanaoishi katika umaskini uliokithiri imeshuka sana kutoka asilimia 11.3 mwaka 2017 hadi asilimia 5.4 mwaka 2024.
Akiwasilisha matokeo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NISR Ivan Murenzi amebainisha kuwa kaya za vijijini ndiyo zilizopunguza zaidi umasikini, ikiashiria athari chanya za sera lengwa za serikali.
Amesisitiza kuwa upanuzi wa upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini, ni ushahidi wa juhudi za maendeleo ya miundombinu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma