

Lugha Nyingine
Maafisa wa Afrika wahimiza juhudi za pamoja kuchochea maendeleo ya bara huku kukiwa na sintofahamu duniani
Maafisa wa Afrika wamesisitiza haja ya kuongeza maradufu juhudi za bara hilo ili kushughulikia changamoto za amani na usalama na kuchochea maendeleo ya Afrika katikati ya kuwepo kwa sintofahamu duniani.
Kauli hiyo imekuja wakati mawaziri wa mambo ya nje wa Afrika, uongozi wa Kamisheni ya Afrika (AU), na maafisa wa vyombo mbalimbali vya AU wakianza kukutana kwenye mkutano wa 24 wa Baraza la Utendaji la AU Jumanne kwenye makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.
Akihutubia kikao cha ufunguzi, Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU Mahmoud Ali Youssouf amesisitiza hitaji la haraka la kuongeza juhudi zinazolenga kuhimiza maendeleo, utulivu, na umoja wa bara hilo ili kuhimili athari mbaya za sintofahamu zinazoendelea kuongezeka duniani.
Naye Waziri wa Mahusiano ya Nje wa Angola ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza Tendaji la AU Tete Antonio, ameunga mkono kauli hiyo, akitilia mkazo hitaji la kushughulikia kwa pamoja changamoto za amani na usalama zinazozuia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Gedion Timothewos, amebainisha jukumu muhimu la AU katika kujenga umoja na dhamira ya bara hilo wakati ambapo Afrika inakumbana na sintofahamu zisizo za kawaida duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma