Algeria yatazamia uhusiano wa karibu wa kiuchumi na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2025

Jukwaa la Biashara kati ya Algeria na China kuhusu Uwekezaji likifanyika Algiers, Algeria, Aprili 15, 2025. (Xinhua)

Jukwaa la Biashara kati ya Algeria na China kuhusu Uwekezaji likifanyika Algiers, Algeria, Aprili 15, 2025. (Xinhua)

ALGIERS - Waziri wa Viwanda wa Algeria Sifi Ghrib amesisitiza uungaji mkono wa serikali ya nchi hiyo kwa ubia kati ya wawekezaji wa China na Algeria ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.

Ghrib ametoa kauli hiyo Jumanne wakati akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Jukwaa la Biashara kati ya Algeria na China kuhusu Uwekezaji lililofanyika mjini Algiers.

Kwa mujibu wa waziri huyo, kampuni 1,311 za China zinafanya kazi kwa mafanikio katika sekta mbalimbali za kiuchumi za Algeria, na thamani ya biashara ya pande mbili ilikuwa imefikia dola za kimarekani bilioni 12.5 mwaka 2024.

Mkurugenzi wa Shirika la Kuhimiza Uwekezaji la Algeria (AAPI) Omar Rekkache amebainisha kuwa shirika hilo limeshaidhinisha miradi 42 ya China yenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 4.5 tangu lilipozinduliwa mwaka 2022, ambayo inajumuisha miradi 22 ya uwekezaji wa moja kwa moja na miradi 20 ya ubia.

Jukwaa hilo la Biashara kati ya Algeria na China kuhusu Uwekezaji, lililoandaliwa na AAPI, linalenga kuvutia uwekezaji wa China na kuzidisha uhusiano wa kiuchumi wa pande mbili. Katika jukwaa hilo, mikataba minane ya ushirikiano imetiwa saini kati ya kampuni za Algeria na China katika sekta mbalimbali, zikiwemo za utengenezaji magari na kilimo.

Wawakilishi kutoka kampuni za Algeria na China wakitia saini makubaliano kwenye Jukwaa la Biashara kati ya Algeria na China kuhusu Uwekezaji mjini Algiers, Algeria, Aprili 15, 2025. (Xinhua)

Wawakilishi kutoka kampuni za Algeria na China wakitia saini makubaliano kwenye Jukwaa la Biashara kati ya Algeria na China kuhusu Uwekezaji mjini Algiers, Algeria, Aprili 15, 2025. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha