Xi atoa maoni matatu juu ya kujenga jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja ya kimkakati na ya kiwango cha juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 17, 2025

Rais wa China Xi Jinping akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim mjini Putrajaya, Malaysia, Aprili 16, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

Rais wa China Xi Jinping akishikana mkono na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim mjini Putrajaya, Malaysia, Aprili 16, 2025. (Xinhua/Huang Jingwen)

PUTRAJAYA, Malaysia - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatano kwenye mkutano wake na Waziri Mkuu wa Malaysia Anwar Ibrahim ametoa maoni matatu kuhusu kujenga jumuiya ya China na Malaysia yenye mustakabali wa pamoja iliyo ya kimkakati na ya kiwango cha juu.

Kwanza, Rais Xi amehimiza nchi hizo mbili kujitawala kimkakati na kufanya ushirikiano wa kimkakati wa ngazi ya juu. China na Malaysia zote zinapaswa kushikilia kujitegemea na kujiimaishwa, na zinapinga kithabiti uingiliaji kutoka nje.

"Nchi hizi mbili zinapaswa kuendelea kushirikiana bega kwa bega katika kufuata njia za maendeleo zinazolingana na hali halisi ya kila moja kati yao, kuungana mkono kithabiti katika kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo, na kushika kwa nguvu mustakabali wao mikononi mwao ," amesema.

Pili, China na Malaysia zinapaswa kukusanya nguvu za maendeleo kwa pamoja, na kuweka mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa maendeleo bora ya hali ya juu. China inajikita katika kujiendeleza kwa sifa bora ya juu ili kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China katika mambo yote, ambayo yanafanana na mpango wa Malaysia wa Ekonomi MADANI.

Tatu, Rais Xi ametoa wito kwa pande zote mbili kurithisha urafiki wao kizazi hadi kizazi na kuzidisha mawasiliano na kufundishana kati ya nchi hizo mbili zenye ustaarabu mbalimbali.

"China na Malaysia zinapaswa kushirikiana katika mazungumzo ya ustaarabu wa Confucius na Uislamu ili kwa pamoja kujenga jukwaa la mawasiliano ya kitamaduni katika ngazi ya pande mbili na kikanda," Kutumia fursa ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusameheana visa, pande hizo mbili zinapaswa kuendeleza kwa hamasa kubwa mawasiliano katika utalii, vijana na serikali za mitaa, na kuzidisha ushirikiano katika utamaduni, elimu, michezo, filamu na vyombo vya habari ili kuongeza maelewano kati ya watu na watu na kuendeleza urafiki wa jadi.

Rais Xi amesema kuwa Malaysia imeweka kaulimbiu ya uenyekiti wa ASEAN mwaka huu kuwa "Ujumuishi na Uendelevu," ambayo inaonyesha ufahamu wa kina juu ya hali ya hivi sasa.

Rais Xi amesema, China inaunga mkono Malaysia katika kutekeleza jukumu lake ikiwa nchi mwenyekiti wa zamu wa ASEAN, na China inapenda kushirikiana na nchi za kanda hiyo kutia saini mapema iwezekanavyo makubaliano ya kupanda ngazi ya Eneo la Biashara Huria kati ya China na ASEAN.

Rais Xi amehimiza kufanya juhudi za pamoja za kukataa kutengana, uvurugaji wa usambazaji bidhaa, "yadi ndogo, uzio mrefu" na utozaji mbaya ovyoovyo wa kodi, na kuvijibu hivyo vyote kwa ujumuishaji, mshikamano na ushirikiano.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Anwar amesema anakaribisha kwa furaha kubwa ziara hiyo ya Rais Xi nchini Malaysia, akiongeza kuwa China imekuwa ikiiunga mkono Malaysia kwa dhati kwa muda mrefu, kusaidiana na Malaysia katika taabu na dhiki katika nyakati za tulivu na mbaya, na China ni rafiki wa kuaminika wa Malaysia.

Amesema kuwa Rais Xi ni kiongozi bora katika dunia ya leo, anayeiongoza China kupata maendeleo makubwa, kuwaongoza watu wa China kuondoa umaskini, na kutetea ustawi wa pamoja na kufundishana kati ya nchi zenye ustaarabu mbalimbali.

Jioni ya siku hiyo, Waziri Mkuu Anwar alifanya dhifa ya kumkaribisha Rais Xi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha