Rais wa DRC ahimiza umoja wa Afrika kwenye mkutano wa mawaziri wa AfCFTA

(CRI Online) April 16, 2025

Mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri wa Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika (AfCFTA) umefunguliwa rasmi jana Jumanne mjini Kinshasa, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku kukiwa na wito mkubwa kutoka kwa Rais Felix Tshisekedi wa nchi hiyo kwa ushirikiano wa kina kwa bara hilo.

Kwenye hotuba yake ya ufunguzi, Rais Tshisekedi amehimiza viongozi wa Afrika kukusanya rasilimali na kuratibu juhudi za kugeuza matarajio ya pamoja ya bara hilo kuwa uhalisia kwa raia wa Afrika.

Rais Tshisekedi ameangazia faida za kimkakati za makubaliano hayo ya biashara huria, zikiwemo za kupanuka ufikiaji wa soko la kikanda, kuchangia teknolojia, uhamishaji ujuzi, na kuendeleza minyororo ya thamani ya kikanda.

Ili kulifanya eneo hilo la biashara huria la Afrika kuwa mafanikio, Rais Tshisekedi ametoa wito zaidi kwa nchi zote za Afrika kuwekeza katika miundombinu ya kuvuka mipaka, kurahisisha na kuwianisha kanuni, na kuunga mkono biashara katika kuingia kwenye soko hilo la bara la Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha