

Lugha Nyingine
Wanamgambo wa RSF wa Sudan watangaza "serikali sambamba" kwenye kumbukumbu ya miaka miwili ya vita
Kamanda wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) nchini Sudan, Mohamed Hamdan Dagalo ametangaza kuunda "serikali sambamba," ambayo amesema “itawakilisha katiba ya kisiasa na katiba ya kihistoria ya mpito kwa Sudan mpya”.
"Serikali sambamba" itaanzisha sarafu mpya na kutoa nyaraka za vitambulisho vya taifa, Dagalo amesema kwenye hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kwenye mtandao wa Telegram, akitoa wito kwa Umoja wa Afrika kuitambua “serikali hiyo sambamba”.
Tangazo hilo limegongana na kumbukumbu ya miaka miwili tangu kuanza kwa vita vya Sudan jana Jumanne.
Aidha, limekuja karibu miezi miwili baada ya kundi la RSF na washirika wake wa kisiasa na kijeshi kusaini makubaliano ya kisiasa mjini Nairobi, yenye lengo la kuanzisha serikali sambamba nchini Sudan.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma