Madaktari wa China wazawadia watoto wa Zanzibar tabasamu jipya kupitia upasuaji wa mdomo wa sungura

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 16, 2025

Fang Jin (katikati), daktari wa upasuaji wa mdomo pamoja na kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania akifanya upasuaji wa mdomo wa sungura na wenzake wenyeji visiwani Zanzibar, Tanzania, Aprili 11, 2025. (Kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar /kupitia Xinhua)

Fang Jin (katikati), daktari wa upasuaji wa mdomo pamoja na kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania akifanya upasuaji wa mdomo wa sungura na wenzake wenyeji visiwani Zanzibar, Tanzania, Aprili 11, 2025. (Kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar /kupitia Xinhua)

DAR ES SALAAM - Kundi la 34 la timu ya madaktari wa China visiwani Zanzibar, Tanzania hivi karibuni imekamilisha pasuaji tano za mdomo wa sungura na pasuaji 19 za kaakaa lililopinda kwa watoto ndani ya siku tano tu -- kila upasuaji umefanywa bila matatizo -- zikirejesha afya na kuwazawadia tabasamu.

Upasuaji huo ulikuwa ni sehemu ya Wiki ya Upasuaji wa Mdomo wa Sungura na Kaakaa Lililopinda, ya siku tano, yenye kaulimbiu ya "Safari ya Tabasamu," iliyoandaliwa na timu hiyo ya madaktari wa China ili kuboresha afya ya wagonjwa, kunufaisha utaalamu wa matibabu, na kuimarisha ushirikiano na wenzao wa Tanzania.

Miongoni mwa wagonjwa hao watoto ni Ibrahim Abdulnassir Ramadhan, mtoto wa mwaka mmoja kutoka Zanzibar. Akiwa alizaliwa na mdomo wa sungura, Ramadhani alikuwa akikabiliwa na matatizo ya kushindwa kunywa maziwa na mara kwa mara alikuwa akilia kwa sababu ya kukosa utulivu. Wazazi wake wamekuwa wakitafuta sana msaada lakini walihofia kuwa wasingeweza kamwe kumudu matibabu hayo.

"Nilipomshika kwa mara ya kwanza, nililia, si kwa sababu ya hali yake, lakini kwa sababu niliogopa dunia isingekuwa na huruma kwake," anasema Raya Rashid Omar, mama wa mtoto huyo. "Watu walimkodolea macho. Wengine hata waliniambia nimfiche, sikutaka huruma, nilitaka tu msaada."

Matumaini yao yaligeuka kuwa uhalisia walipofahamu kuhusu "Safari ya Tabasamu" hiyo iliyoongozwa na Wachina. Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali, mtoto huyo alichaguliwa kufanyiwa upasuaji katika Hospitali ya Lumumba.

"Nilikuwa na wasiwasi, yeye ni mdogo sana," anasema Abdulnassir Ramadhan Suleiman, baba wa mtoto huyo, huku akitazama timu ya madaktari ikiwa imembeba mtoto wake kuelekea chumba cha upasuaji. "Lakini madaktari walimtazama jinsi tunavyomtazama. Walimwona mtoto anayestahili maisha ya baadaye."anaongeza.

Wakiongozwa na Fang Jin, daktari wa upasuaji wa mfumo wa mdomo kutoka timu hiyo ya madaktari ya China, upasuaji uliendelea vizuri. Fang alifanya kazi pamoja na madaktari watatu wenyeji kutoka mji mkuu, Dodoma. Kwa pamoja, waliunda timu ya wataalamu iliyoshirikiana vyema.

Katika kipindi kizima cha siku hizo tano, timu hiyo ilifanya kazi bila kuchoka, ikifanya kila upasuaji kwa usahihi na uangalifu. Baada ya upasuaji, walifanya ukaguzi wa kila siku ili kufuatilia hali ya kupona kwa afya na kuhakikisha matokeo bora iwezekanavyo.

Ramadhani alipoamka kutoka kwenye upasuaji huo, wazazi wake walishindwa kuzuia hisia zao.

"Kwa mara ya kwanza nimeona tabasamu lake bila maumivu," mama huyo anasema huku akizuia machozi. "Alionekana kama alikuwa akingojea kila wakati kuwa mwonekano wake wa sasa."

Mageuzi hayo si tu yamegusa wafanyakazi wa matibabu bali pia watu wa kujitolea katika Hospitali hiyo ya Lumumba. Watoto wengi, ambao hapo awali walikuwa na haya au kimya, walianza kucheza na kuchekawakiwa na nyuso zao mpya zilizopona.

Fang amekumbushia wakati ambapo mama alimshika mkono wake kwa nguvu baada ya upasuaji huo. "Hakusema mengi. Alisema tu 'daktari wa China, asante.' Lakini macho yake yalisema kila kitu, "anasema.

Wataalamu wa matibabu wenyeji pia wameelezea juu ya hali ilivyokuwa. "Ushirikiano huu na timu ya China umekuwa wa kutufungua macho. Si tu tumejifunza mbinu za hali ya juu bali tumeshuhudia jinsi huruma inavyoonekana katika utendaji," amesema Seseja, mmoja wa madaktari watatu wa Tanzania.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha